• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda yakumbusha tena madai ya Afrika ya mageuzi ya Umoja wa mataifa

    (GMT+08:00) 2015-10-08 10:21:20

    Rais Yoweri Museveni wa Uganda amekuwa akisafiri katika nchi mbalimbali duniani kuzishawishi kuhusu ufuatiliaji wa nchi za Afrika ili kuendelea kuhimiza amani na usalama duniani. Kuanzia Japan, China na hata kwenye Umoja wa Mataifa, Rais Museveni amekuwa akihimiza msimamo wa Afrika wa kuwa na kiti kwenye baraza la usalama la umoja wa mataifa, unaojulikana kama makubaliano ya Ezulwini.

    Mwaka 2005 nchi za Afrika zilifikia msimamo wa pamoja kuhusu mageuzi ya Umoja wa mataifa, unaoitwa Ezulwini, ukitaka Afrika iwe na wajumbe wawili wa kudumu na wajumbe watano wasio wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa mataifa, na kuzipa nchi hizo haki ya kupiga kura ya turufu.

    Kwa sasa baraza la usalama la Umoja wa mataifa lina wajumbe watano wa kudumu ambao ni Uingereza, Marekani, Ufaransa, Russia na China. Lakini nchi za Afrika zimekuwa zikisema mwaka 1945 Umoja wa mataifa ulipoanzishwa, nchi nyingi za Afrika hazikuwakilishwa, na mwaka 1960 wakati mageuzi yalipofanyika kwenye umoja wa mataifa Afrika iliwakilishwa, lakini uwakilishi wake haukuwa na nguvu. Kwa hiyo bara la Afrika sasa linataka kuwakilishwa kikamilifu kwenye vyombo vya maamuzi vya Umoja wa mataifa na hasa baraza la usalama, ambalo hufanya maamuzi yote yanayohusiana na amani na usalama duniani.

    Katibu Mkuu wa wizara ya mambo ya nje ya Uganda Bw James Mugume amesema nchi nyingine zimekuwa zikiishawishi Afrika iiunge mkono, kwa hiyo anaona Afrika nayo iko huru kuzishawishi nchi nyingine.

    Katika ziara aliyofanya miezi minne iliyopita nchini Japan, Rais Yoweri Museveni wa Uganda alilaumu kuwa migogoro ya kisiasa iliyopo duniani kwa sasa inatokana na baadhi ya kuhodhi ufanyaji wa maamuzi, na pia alilaumu baraza la usalama la Umoja wa mataifa katika suala la msukosuko wa wakimbizi unaoikabili Ulaya kwa sasa.

    Rais huyo ameonya kuwa kama kama Umoja wa Mataifa usipo kuwa na tahadhari, unakuwa uwanja wa watu wengine kutafuta maslahi yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako