• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalamu wanasema athari ya TPP kwa China ni ndogo

    (GMT+08:00) 2015-10-08 18:46:56

    Baada ya mazungumzo magumu ya biashara yaliyodumu kwa miaka mitano, Marekani na nchi nyingine 11 zikiwemo Australia na Japan zilifikia Makubaliano ya Uhusiano wa Kiwenzi kati ya Nchi za Ukanda wa Bahari ya Pasifiki TPP. Hii inamaanisha kuwa kama Makubaliano hayo yatapitishwa katika nchi hizo, mtandao mkubwa wa kiuchumi unaojengwa kwa msingi wa kanuni mpya za kibiashara kati ya nchi zinazochangia asilimia 40 ya uchumi wa dunia utaanzishwa, na hakika Makubaliano hayo yatatoa athari za moja kwa moja kwa biashara ya China na nchi za nje. Hata hivyo wataalamu wanaona kuwa athari hizo ni ndogo, na China inatakiwa kuhimiza kwa nguvu mazungumzo kuhusu kuanzishwa kwa maeneo ya biashara huria ya Asia na Pasifiki.

    Makubaliano ya TPP yanaongozwa na Marekani, na mazungumzo husika yalianzishwa miaka mitano iliyopita. Kuna Nchi 12 zinazoshirikishwa kwenye makubaliano hayo, ambazo zinachukua asilimia 40 ya uchumi wa dunia, kiasi ambacho kinazidi Umoja wa Ulaya. Baadhi ya watu wanasema TPP ni hatua ya Marekani ya "kuleta uwiano mpya katika Asia na Pasifiki", na wengine wanaona TPP inalenga kujenga "NATO ya kiuchumi" barani Asia. Akizungumzia kukamilishwa kwa mazungumzo hayo, msemaji wa Wizara ya Biashara ya China Yao Jian amesema China ina "msimamo wazi" na ujenzi wa utaratibu wowote unaoendana na kanuni za Shirika la Biashara Duniani na kuchangia mafungamano ya kiuchumi ya kanda ya Asia na Pasifiki. Kuhusu kauli hiyo, naibu mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kimataifa ya China Ruan Zongze anasema,

    "Marekani inalenga kupata uongozi katika uchumi na utungaji wa kanuni za kiuchumi na kibiashara kupitia TPP. Kama alivyosema msemaji wa Wizara ya Biashara, China ina msimamo wazi, na kwamba kwanza China haizuii TPP, pili athari zinazoweza kutokana na TPP kwa China na utaratibu wa biashara ya pande nyingi duniani zinahitaji kuchunguzwa zaidi. Kwa ufupi tunatarajia kuwa TPP inaweza kuchangia maendeleo ya mafungamano ya kiuchumi katika Asia na Pasifiki."

    Makubaliano ya TPP yakianza kutekelezwa, biashara kati ya nchi wanachama zitafanywa kwa ushuru mdogo au bila ushuru, hali hii hakika itakuwa na athari kwa China ambayo iko nje ya Makubaliano hayo. Lakini wataalamu wanaona athari itakuwa ndogo. Mkurugenzi wa ofisi ya ushirikiano wa kimataifa ya taasisi ya utafiti wa uchumi na nje iliyo chini ya Kamati ya taifa ya Maendeleo na Mageuzi ya China Zhang Jianping anasema,

    "Hadi sasa China imesaini makubaliano ya biashara huria ya pande mbili na theluthi mbili ya nchi wanachama wa TPP, hali inayoweza kupunguza athari mbaya za TPP. Aidha Kama Makubaliano ya Uhusiano Mpana wa Wenzi wa Kiuchumi ya Kikanda RCEP yanayohusisha nchi 16 zikiwemo nchi 10 za Umoja wa Nchi za Kusini Magharibi mwa Asia, China, Japan na Korea Kusini pamoja na Australia, Singapore na India yanaweza kuanzishwa, kwa kiasi fulani yanaweza kuondoa athari mbaya kwa biashara ya kigeni ya China na kipato cha wananchi wake."

    Wataalamu pia wametoa wito kwa China kuendelea kufanya juhudi ili kufikia makubaliano ya ngazi ya juu ya biashara huria ya pande mbili na ya kikanda, na kukamilisha hatua kwa hatua utaratibu mpya wa uchumi wazi. Naibu mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kimataifa ya China Ruan Zongze anasema,

    "Watu wanafuatilia sana athari mbaya zinazotokana na TPP kwa China. Lakini naona China inapaswa kuendelea kusukuma mbele mipango kuhusu makubaliano ya biashara huria ya pande mbili na ya kikanda. Hivi sasa China imefikia makubaliano ya biashara huria au inafanya mazungumzo husika na makumi ya nchi duniani, hatua hizo zimeongeza uwezo wa China katika kukabiliana na athari zenye utatanishi. Pili, China inatakiwa kuharakisha mazungumzo kuhusu eneo la biashara huria la Asia na Pasifiki, kwani tumetambua kuwa kanda hiyo ina makubaliano ya TPP, RCEP, 10+1, 10+3, n.k. Kutumia makubaliano ya eneo la biashara huria la Asia na Pasifiki kuunganisha makubaliano hayo mbalimbali ni kazi muhimu katika kuendeleza mafungamano ya kiuchumi katika kanda ya Asia na Pasifiki."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako