• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kutekeleza alama maalum ya takwimu ya IMF ili kuongeza uwazi

    (GMT+08:00) 2015-10-08 19:05:20

    Takwimu rasmi za China zitafuata utaratibu wa SDDS ulioanzishwa na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF ili kuimarisha uwazi.

    Baada ya kupitishwa na baraza la serikali la taifa, gavana wa Benki Kuu ya China Zhou Xiaochuan alimwarifu mkurugenzi mkuu wa IMF Bi. Christine Lagarde kuhusu uamuzi huo wa China.

    Tangu mwaka 2002, China ilikuwa inatumia mfumo wa GDDS, ambao ulianzishwa na IMF mwezi Disemba mwaka 1997, ili kutoa mwongozo kwa nchi kufuata na kuboresha mfumo wa takwimu. Mfumo huu unatumika kwa nchi zote wanachama wa IMF, bali mfumo wa SDDS unatumiwa na nchi ambazo tayari zina masoko ya nje au zinatafuta masoko hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako