• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  •  China yachukua nafasi kubwa katika kuinua ushirikiano wa Kusini-Kusini

    (GMT+08:00) 2015-10-09 16:02:34

    Mkurugenzi wa Mkutano wa Biashara na Maendeleo wa Umoja wa Mataifa UNCTAD kanda ya Afrika Tesfachew Taffere amesema, China ina nafasi muhimu katika kuinua ushirikiano wa Kusini-Kusini kupitia kuimarisha miundombinu muhimu katika nchi zinazoendelea.

    Taffere amesema, China imejenga miundombinu muhimu katika nchi zinazoendelea, hususan kwenye sekta ya nishati na usafiri, ambayo ni muhimu kwa biashara na shughuli nyingine za kiuchumi. Ofisa huyo pia ameielezea China kama mfano kwa nchi nyingine kutokana na mafanikio yake katika maendeleo na mapambano dhidi ya umasikini. Taffere amesema katika miongo miwili, China imetimiza kupunguza umasikini kwa mamilioni ya watu, na kwamba nchi hiyo ni mfano kwa nchi nyingine zinazoendelea.

    Katika mkutano wa Umoja wa Mataaifa kuhusu Maendeleo Endelevu uliofanyika mjini New York mwishoni mwa mwezi uliopita, rais Xi Jinping wa China aliahidi kuwa China itatoa dola za kimarekani bilioni 2 kuunga mkono nchi zinazoendelea katika kutimiza malengo ya maendeleo ya Umoja wa Mataifa baada ya mwaka 2015. Taffere amepongeza pendekezo la China la kuunga mkono nchi zinazoendelea katika mchakato wao wa kutimiza lengo la dunia nzima la kuondoa umasikini ifikapo mwaka 2030.

    Amesema hivi sasa China imekuwa alama ya kile ambacho nchi zinazoendelea zinaweza kutimiza, na amesema China inawajibika na pia inatakiwa kuhakikisha kuwa utajiri wake pia unazinufaisha nchi nyingine kupitia malengo hayo ya maendeleo ya dunia. Amesema njia moja ya kuzisaidia nchi zinazoendelea ni kuhakikisha kuwa zinatimiza, japo kwa wakati huu, malengo haya ya maendeleo endelevu.

    Taffere amesema, nchi nyingi zenye hali mbaya ya kiuchumi, hususan zilizo nyuma zaidi kimaendeleo, zilikabiliwa na changamoto kubwa ya kutimiza Malengo ya Maendeleo ya Milenia ya Umoja wa Mataifa. Lakini anatumai kuwa, mpaka kufikia mwaka 2030, nchi nyingi zitaonyesha alama ya wazi ya kuondokana na umasikini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako