• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ban Ki-moon apongeza wajumbe waliopendekezwa kuunda kamati ya rais nchini Libya

    (GMT+08:00) 2015-10-09 16:56:38

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon amepongeza orodha ya wajumbe waliopendekezwa kwenye kamati ya rais, ambao watasaidia kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya.

    Taarifa iliyotolewa na msemaji wa katibu mkuu huyo Stephane Dujarick imesema, Ban amewasifu washiriki wa mjadala huo kwa kufikia waraka kamili wa makubaliano ya kisiasa baada ya majadilio ya kina na ya pande zote. Ban amezitaka pande mbalimbali ziunge mkono pendekezo hilo, na kusaini makubaliano haraka .

    Mjumbe maalum wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Libya ambaye pia ni kiongozi wa tume maalum la Umoja wa Mataifa nchini humo Bernardino Leon, jana usiku mjini Skhirat nchini Morocco alitangaza kuwa, Libya itaunda serikali ya umoja wa kitaifa inayoongozwa na waziri mkuu Faizi Sarraj.

    Leon amesema, mbali na Sarraj, Umoja wa Mataifa pia uliteua naibu waziri mkuu 3 na waziri 2 wa ngazi ya juu, ili kuunda kamati ya rais.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako