• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Balozi wa China kwenye Umoja wa Mataifa atoa mapendekezo ya utekelezaji wa ajenda za maendeleo baada ya mwaka 2015

    (GMT+08:00) 2015-10-09 16:57:37

    Naibu balozi wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Wang Min ametoa mapendekezo kwa kamati ya pili ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu utekelezaji wa ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015 ili kutoa mchango kwa maendeleo na ustawi wa dunia.

    Bw. Wang amesema, nchi mbalimbali zinatakiwa kuwajibika na majukumu ya kutekeleza ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015, kuzingatia kuondoa umaskini na kupata maendeleo, kuimarisha uhusiano wa wenzi wa maendeleo, kuongeza ushirikiano wa kusini na kusini, na kuboresha maendeleo ya kimataifa. Pia kushirikiana zaidi katika kukabiliana na masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa, usalama wa chakula na nishati.

    Amesema, ongezeko la uchumi wa China litatoa fursa zaidi kwa soko, uwekezaji na ushirikiano wa dunia. Pia China itaendelea kutekeleza dhana mpya ya maendeleo iliyotolewa na rais Xi Jinping wa China ambayo ni ya haki, uwazi, ukamilifu na uvumbuzi, na kusukuma mbele maendeleo ya dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako