• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa biashara wa China asema China inaendelea na mawasiliano kati yake na nchi wanachama wa TPP

    (GMT+08:00) 2015-10-09 16:57:43

    Waziri wa biashara wa China Gao Hucheng amesema, China na nchi wanachama za Makubaliano ya Uhusiano wa Kiwenzi kati ya Nchi za Ukanda wa Bahari ya Pasifiki TPP zinaendelea kuwasiliana kuhusu mazungumzo mbalimbali ya biashara huria yanayofanyika katika nchi hizo.

    Waziri huyo amesema hayo baada ya Marekani na nchi nyingine 11 kutangaza kufikia makubaliano ya TPP. Bw. Gao amesema siku zote China inaona na kusisitiza kuwa makubaliano kuhusu biashara huria yaliyofikiwa na yanayojadiliwa sasa katika kanda ya Asia na Pasifiki yakiwemo TPP, ni njia muhimu inayohimiza uhuru na urahisi wa biashara na uwekezaji, kusukuma mbele utandawazi wa kikanda na maendeleo ya uchumi katika kanda hiyo, na kuchangia maendeleo endelevu ya uchumi wa dunia.

    Akitaja athari ya TPP kwa China Bw. Gao amesema China itafanya tathmini kwa pande zote na utaratibu kwa kufuata makubaliano hayo yatakayotolewa rasmi na pande husika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako