• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kujenga vituo vya kuongezea nishati kwenye gari

    (GMT+08:00) 2015-10-09 18:50:23

    China imetangaza mipango ya kujenga vituo vya kuongezea nishati kwenye betri za gari za stima zipatazo milioni 5 ambazo zitatumika nchini humo ifikapo mwaka wa 2020.

    Taarifa ya baraza kuu la China inasema mpango huo utahusisha maeneo ya makazi, ya kibiashara, na barabara kuu.

    Majengo mapya ya makazi yatatakiwa kuwa na maeneo ya kuongezea nishati ama kuacha nafasi kwa ajili ya vifaa hivyo. Maeneo ya kuegesha magari pia yanatakiwa kuwa na asilimia 10 ya nafasi iliotengwa ili kutumika kwa shughuli hiyo.

    Ili kufadhili mradi huo, serikali inawaalika wawekezaji wa kibinafsi, kuwakubalia wategenezaji wa vifaa hivyo kutoa bodi na pia kutafuta uwekezaji kutoka kwa hazina ya uzeeni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako