• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yataka sekta binafsi kushiriki kwenye miradi mikubwa

    (GMT+08:00) 2015-10-09 19:56:39

    Serikali ya Tanzania imeihimiza sekta binafsi kushiriki katika miradi mikubwa, chini ya utaratibu wa ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP).

    Akizungumza mjini Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha nchini Tanzania Profesa Adolf Mkenda amesema kuna sheria inayoongoza ubia kati ya sekta ya umma na binafsi, hivyo hakuna sababu ya sekta binafsi kusitasita katika kushiriki miradi mikubwa.

    Ameongeza kuwa nchi nyingi zilizoendelea, hasa katika sekta ya miundombinu, zimeshirikisha zaidi sekta binafsi kwenye miradi mikubwa na kuzisaidia nchi hizo kukuza uchumi kwa kasi.

    Amefafanua kuwa fursa hizo ziko wazi kwa wajasiriamali Watanzania na wageni, na kuongeza kuwa suala kubwa ni utoaji wa huduma bora na yenye ufanisi.

    Kwa upande wake, mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Godfrey Simbeye amepongeza msukumo huo wa serikali na kueleza sekta binafsi ina nia ya kutumia fursa hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako