• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wadau wa Utalii wataka shirika la Feli Kenya kupunguza ada za kuvukisha magari

    (GMT+08:00) 2015-10-09 19:56:54

    Wadau katika sekta ya utalii nchini Kenya wameitaka shirika la Feri nchini Kenya kupunguza ada za kuvukisha magari katika kivuko cha Likoni nchini Kenya hadi chini ya asilimia saba badala ya zaidi ya asilimia 50. Chama cha watoaji huduma za kusafirisha watalii KATO na chama cha watoaji huduma za hoteli kimetaka shirika hilo lianze kutoza ada hizo ambazo wamependekeza kuanzia Aprili mwaka ujao. Mwezi uliopita, mkurugenzi mkuu wa KFS Musa Hassan Musa alisema shirika hilo linalazimika kupandisha ada za kuvukisha magari baada ya hazina kuu kupunguza bajeti yake kutoka shilingi milioni 300 hadi 230. Hata hivyo Bw Musa amesema KFS inatarajia kukusanya shilingi milioni 52 kama itaidhinisha ada ilizopendekeza kwa wanaotumia huduma za feri.Mwenyekiti wa KATO Monika Solanki amesema wadau wa Utalii walishangazwa na mapendekezo ya KFS ya kuongeza ada za kuvukisha magari kwa kati ya asilimia 59 na 62.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako