• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ujenzi wa eneo maalum la kiviwanda nchini Ethiopia waanza.

    (GMT+08:00) 2015-10-09 19:57:10

    Kampuni ya China ya CCECC maarufu kama China Civil Engineering sasa imeanza rasmi ujenzi wa eneo maalum la viwanda nchini Ethiopia.

    Ujenzi wa eneo hilo ulikuwa umetangazwa na serikali ya nchi hiyo mapema mwezi wa nane.

    Eneo hilo linajengwa katika eneo la Hawassa na kwa mujibu wa wizara ya biashara na viwanda nchini humo ni kwamba ujenzi wake utagharimu Dola milioni 246 za kimarekani.

    Mradi huo katika awamu ya kwanza kutakuwa na majumba 19 ya viwanda, na katika awamu ya pili majumba 19 ya ofisi, malazi na mighahawa midogo midogo.

    Kufikia sasa kuna maeneo manne maalum ya kiviwanda katika nchi ya Ethiopia na serikali inasema inapanga kuendelea kuongeza maeneo hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako