• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sanaa ya uchongaji wa mawe ya Soapstone huko Kisii, magharibi mwa Kenya

    (GMT+08:00) 2015-10-21 08:48:49

    Mawe ya Soapstone pia yanaitwa mawe ya Kisii, ambapo jina hilo linatokana na jina la kabila la Kisii linaloishi kwenye eneo la milima ya Tabaka, magharibi mwa Kenya. Watu wa kabila hilo wameanza kutumia mawe hayo mapema, na katika miaka ya karibuni tu wameanza kuchonga mawe hayo kwa ajili ya biashara. Ustadi hodari wa kuchonga wa wasanii wa Kisii umesaidia sana kujenga umaarufu wa vinyago vya Soapstone.

    Zamani wasanii wa Kisii walipenda kuchonga vinyago vya wanyama tu, lakini hivi sasa wameanza kuchonga vitu vya matumizi ya kisasa, kama vile vishikizo vya mshumaa, vifaa vya kushikilia vitabu na kadhalika.

     

    Kabla ya kuchonga, wasanii kwanza huweka mawe ya Sopestone majini ili kuyalainisha zaidi yaweze kuchongwa kwa urahisi, na baada ya kukauka, mawe hayo yanafanya umbo lililochongwa lidumu zaidi. Halafu wanapaka rangi sanamu walizochonga ili kuzifanya zing'are zaidi.

    Kutokana na kuwa mchakato mzima wa uchongaji wa vinyago vya mawe ya Sopestone unategemea mikono, kwa hiyo ufanisi wa kazi hiyo ni wa chini sana. Lakini hali pia inahakikisha kuwa sanaa hiyo ina umaalumu wake wa kipekee.

    Karibu na eneo la Tabaka magharibi mwa Kenya, kuna sehemu maarufu kwa ajili ya shughuli za uchongaji wa mawe ya Soapstone. Vizazi vya Tabaka vimepokezana utamaduni wa uchongaji kwa miaka mingi na karibu kila nyumba ina msanii. Mmoja wa wakazi wa hapa kwenye eneo linalochimbwa mawe ni David Osase na amekuwa kwenye eneo hilo kwa zaidi ya miaka 39. Alisema, Kazi yake ni kuchonga tu na anaitegemea sana kazi hiyo.

    Sio mawe yote ambayo yanafaa kwa shughuli za uchongaji. Hivyo kabla ya kuanza kuchonga vinyago wasanii kwanza huyakagua. Yasiyofaa kuchongwa hutumiwa katika ujenzi wa nyumba na barabara.

    Katika mji mdogo wa Tabaka kuna ofisi ya chama cha wasanii wa kuchonga.

    Hapa zinafanyika shughuli za kuuuza vinyago kwenye soko la Kenya na hata nje ya nchi.

    Ofisi hii ilianzishwa mwaka wa 1965. Bw Evans Igoge ni mmoja wa wanachama wa chama cha wasanii. Amesema, Kazi ambayo wanafanya huko ni kupokea bidhaa kutoka kwa wachongaji, wanazipakia vizuri na kuzituma nchi za nje.

    Bw Elkana Ogesa ni msanii mtajika ambaye sanamu zake zimeshinda tuzo nyingi za kimataifa. Ogesa ndiye mwenyekiti wa chama hiki cha wasanii hapa Tabaka. Anasema mgao wa soko la bidhaa zao kimataifa ni mdogo lakini wanafanya kila juhudi kupanua soko lao katika nchi za nje kama vile China. Amesema, Kwa wakati huu bado ni dogo kwa sababu hawajui mambo mengi kulingana na hali ya soko la kimataifa. China ni nchi kubwa yenye watu wengi ambayo wanaweza kupata soko, kwa hivyo wanataka kuwasiliana na tayari wamezungumza na ubalozi wa China nchini Kenya.

    Uchongaji wa sanamu katika eneo hili la Tabaka sio tu umesaidia kuhifahi utamaduni wa jamii ya wakisii lakini pia umekuwa kivutio cha utalii.

     

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako