• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hadithi za shamba la familia ya Zhang Tian

    (GMT+08:00) 2015-10-26 10:19:22

    Kwa muda wa mwaka mmoja na nusu uliopita, hapa China, kampuni zaidi ya elfu 10 zinaanzishwa kila siku. Na hivyo, wimbi la "kuanzisha biashara na kuwa na uvumbuzi kwa wengi" limekuwa nguvu mpya ya kusukuma mbele maendeleo ya uchumi wa China.

    Wanawake wa China vilevile wanashiriki kwa wingi katika wimbi hilo, ikiwa ni hatua ya kujipitia maisha bora zaidi, na pia wanachangia maendeleo ya uchumi wa nchi yao. Lakini katika mchakato wa kuanzisha biashara, wanawake wa China wanakabiliwa na changamoto na matatizo gani? Changamoto na matatizo hayo yanaweza kutatuliwa kwa kupitia njia gani?

    Majibu ya maswali hayo Pili tutayapata katika mfululizo wa vipindi hivi vitatu kuhusu wanawake wa vijijini hapa China, kwani waandishi wetu walitembelea miji mitatu iliyoko mashariki na magharibi mwa China, na kufanya mahojiano na wanawake wa huko.

    Hili ni shamba moja lililoko eneo la Tongnan kusini magharibi mwa mji wa Chongqing, hapa China. Shamba hilo linaitwa "shamba la familia ya Zhiqing", na limeanzishwa na mwanamke aitwaye Zhang Tian. Familia yake inajishughulisha na kilimo cha matunda, hivyo tangu akiwa mdogo, Zhang Tian alipenda sana kuchezea na miti ya matunda, anajua kiasi cha mbolea kinachotakiwa, na hata namna ya kupunguza matawi. Zhang alikuwa na kazi nzuri tu hapa Beijing, lakini mwaka 2012 aliamua kuacha kazi na kurudi nyumbani kuanzisha biashara.

    Kwa msaada wa shirikisho la wanawake la eneo la Tongnan na shirikisho la wanawake la mji wa Chongqing, Zhang alikodi heka 100 ya ardhi kwa lengo la kupanda miti ya matunda, na vilevile alisajili chapa ya shamba la familia la Zhiqing". Zhang anasema wazo la kufanya biashara hiyo alikuwa nalo muda mrefu, lakini lengo lake lilikuwa ni kumpunguzia kadhia baba yake.

    "Wakati ule matunda yalipoiva, nilimuona baba yangu akibeba matunda hayo begani na kwenda kuyauza mjini. Nililia sana kwani mabega yake yalimuuma sana na kutoka damu. Aidha katika majira kama haya, kuna mvua sana, niliona majirani wakitaka kununua vitu mjini, walilazimika kukunja suruali zao na kupita kwenye tope, wakifika mjini, wanasafisha miguu yao na kuvaa viatu. Nilidhani naweza kuletea mawazo fulani, kwa mfano badala ya baba kupeleka matunda mjini, tunaweza kuwavutia watu wa mjini kuja shambani kwetu na kuchuma matunda katika shamba letu la matunda."

    Zhang naye alikumbana nazo. Anakumbuka kuwa mwanzoni yeye na baba yake walichagua aina mpya ya mti wa peasi hapa Beijing, walivyorudi kijijini kwao, walikata miti yote ya matunda zaidi ya heka 10 kwenye shamba lao, na kupanda miti hiyo mipya. Lakini baada ya miaka mitatu, matunda yaliyotokana na miti hiyo yaliwasikitisha sana.

    "Tulishtuka sana. Kwani ukikata miti hiyo inabidi kusubiri miaka mitatu ndipo unaweza kupanda miti mingine. Matunda ya miti ambayo tulipanda yalikuwa ni madogo kuliko tuliyoyaona, na hayakuwa matamu, tukajua kuna pengo kubwa kati ya thamani yake ya kiuchumi na ile tuliyotarajia awali."

    Zhang hakukata tamaa, aliwasiliana na timu ya wataalam wa teknolojia ya kilimo, ambao waligundua kuwa, tatizo liko kwenye ufundi wa kupanda miti ya matunda.

    "Pendekezo lililotolewa na wataalam hao ni kuwa 'tusikate miti iliyopo na kupanda miti mipya, bali tupandikize aina mpya, kujaribu utamu wao, aina yao, thamani yao ya lishe, thamani yao ya kiuchumi, na kama thamani hizo ni za juu, basi tutaongeza ukubwa wa shamba' Hivyo tunayo miti ya mama, iliyopandikizwa, na itaanza kuchipua mwaka ule ule, na mwaka ujao itachanua maua na kuwa na matunda."

    Kutokana na msaada wa wataalam wa teknolojia ya kilimo, uhai mpya ukarejea kwenye shamba la familia la Zhang Tian. Naibu mwenyekiti wa shirikisho la wanawake la eneo la Tongnan Bibi Chen Chunlu anasema, kai kubwa ya wataalam hao ni kuwaunga mkono kiteknolojia wamiliki wa biashara wanawake kama Zhang Tian.

    "Tuna kituo cha kuwafundisha wanawake wanaoanzisha biashara, na kituo cha kufanya mazoezi husika. Shirikisho letu na kamati ya kilimo ya Tongnan ziliunda timu ya wataalam wa teknolojia ya kilimo inayohudumia wanawake, na inashirikisha wataalam zaidi ya 20 sasa. Wataalam hao wanaweza kuwasaidia kukabiliana na matatizo katika mchakato wa uendeshaji wa biashara wakati wowote."

    Mbali na uongozi wa wataalam wa kilimo, Zhang Tian pia alishiriki kwenye mafunzo wa teknolojia yaliyoandaliwa na shirikisho la wanawake la Chongqing kwa "wakulima wa kike wa aina mpya". Ili kueneza elimu na ujuzi wa kilimo alioupata, Zhang Tian alianzisha "shule ya mafunzo shambani" katika shamba lake, ambayo imekuwa jukwaa la kuelimisha na kuwafundisha watu mbalimbali teknolojia ya uzalishaji wa kilimo, kinga na tiba ya magonjwa wa miti ya matunda, na njia ya usimamizi wa miti ya matunda inayopandwa kwenye ndoo maalum.

    "Tunafanya nini? Tunaondoa sehemu zote za katikati, tunatoa jukwaa, na kuunganisha sehemu ya mwisho. Familia moja ikipanda miti ya matunda kwa ekari 10 hivi, tutatoa uongozi wa kiteknolojia, na kuwapa mbegu, kuwafundisha namna ya kupanda miti, halafu wanauza, na kupata fedha, ni hatua tatu tu. Hili ni wazo langu la hatua ijayo."

    Lengo kubwa la mashirika ya wanawake sehemu za vijijini hapa China ni kuwaunga mkono na kuwaongoza kushiriki kwa juhudi kubwa kwenye ujenzi wa kilimo cha kisasa, na kuwapatia mafunzo na misaada kuhusu ufundi wa kupata ajira na kuanzisha biashara. Naibu mwenyekiti wa shirikisho la wanawake la Chongqing Bibi Zhou Mi anafahamisha kuwa:

    "Katika upande wa uungaji mkono wa kielimu, moja ni kuwa timu ya wataalamu wakiwemo wafanyakabiashara waliofanikiwa wanasaidia wanawake wanaoanzisha biashara kwa kuwawasiliana na kutoa mapendekezo na uongozi husika. Nyingine ni kuwa tunaandaa na kutekeleza shughuli mbalimbali za kutoa ushauri moja kwa moja kwa wanawake wanaoanzisha biashara ambao huenda watakumbwa na changamoto mbalimbali. Shirikisho letu linajenga jukwaa la mawasiliano na mazungumzo kati ya wanawake hao na idara husika za serikali."

    Hivi sasa shamba la familia la Zhang Tian limeendelea kutoka kupanda miti ya matunda tu hadi kuwa shamba lenye ekari 200 linalojumuisha kupanda miti ya matunda, kuchuma matunda, sehemu za kupumzika, mkahawa na hoteli. Mama yake Zhang Tian Bibi Mao Jiamei anamsaidia mtoto wake akiwa na wakati, machoni mwake sababu kuu ya maendeleo ya shamba lao ni uongozi wa teknolojia ya kilimo.

    "Wakulima wake waliona sisi tupande miti ya matunda katika mwaka wa kwanza, turutubishe miti katika mwaka wa pili, na tupate matunda katika mwaka wa tatu, wao wana transplant rice seedlings mashambani. Wakulima majirani wakatufuata na kutusomea, wakapanda miti ya matunda vilevile. Wakipanda mtama, watapata nusu kilogram, ni dola za kimarekani 150 hivi tu, lakini sisi tunaopanda miti ya matunda hupata mapato mengi zaidi, mara nyingi sana."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako