• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Simama na kueneza upendo: Bibi Chen Xiuhua mwenye kansa aanzisha biashara kuwasaidia wengine

    (GMT+08:00) 2015-11-16 07:44:32

    Katika kipindi cha leo, tutamzungumzia Bi. Chen Xiuhua.

    "Mimi naitwa Chen Xiuhua, mwaka huu ninatimiza miaka 50, mimi ni mwanamke wa kawaida wa kijijini, nina saratani ya shingo ya uzazi, na iko kwenye hatua ya kati au ya mwisho. Lakini nilibahatika sana, watu wengi walinisaidia. Nilifanya mambo ambayo nilitakiwa kufanya, lakini ninakubaliwa na wote. Familia yangu ilichaguliwa kuwa 'familia 10 bora za Chongqing' na 'familia bora nchini China', na niwakilisha 'familia bora' pekee nchini China, na nilipewa tuzo katika Jumba Kuu la Umma la China."

    Hiyo ni sehemu ya hotuba ya Bibi Chen Xiuhua kwenye hafla ya kutoa tuzo kwa 'familia bora" mwezi Mei mwaka huu. Sasa tuangalie historia yake. Mwaka 2011 Chen Xiuhua aligunduliwa kuwa na kansa ya shingo ya uzazi, kama hiyo haikutosha, siku tatu tu baadaye, baba yake alipooza kutokana na damu kuvuja kwenye ubongo wake. Balaa moja baada ya nyingine yalimkatisha tamaa Chen Xiuhua. Baada ya kukosa utatuzi wa suala hilo, Chen aliamua kwenda shirikisho la wanawake la eneo la Tongnan la mji wa Chongqing kuomba msaada.

    "Wanawake wa shirikisho la hilo waliniunga mkono, kunitia moyo, na kunisaidia kukabiliana na hali ngumu. Wakati ninaondoka, mwanamke mmoja alisema neno moja ambalo lilinitia moyo na kunifanya niendelee na maisha yangu. Alisema : 'Xiuhua, shirikisho la wanawake ndio nyumbani kwa wakwe zako, unakaribishwa hapa wakati wowote.' Kauli hiyo ilinifanya kuamini kuwa ninapaswa kuendelea na maisha kwa moyo imara. Sisi ni wanawake, nahisi nina nyumbani kwa wakwe na dada vilevile. Baadaye nilianza kufuga sungura, hadi sasa naishi kwa furaha kubwa. Kama hakuna mtu anayenikumbusha, huwa nasahau kama mimi kumbe ni mgonjwa, ni kweli."

    Mwenyekiti wa shirikisho la wanawake la eneo la Tongnan Bibi Dai Hongli anakumbuka mara ya kwanza alipomuona Chen Xiuhua:

    "Tuliongea naye maneno machache tu, lakini alisikia na kukubali. Tulisema: 'ukiwa na sura ya huzuni namna hii, ndugu zako hawafurahi kabisa. Lakini ukitabasamu kila siku, kufanya vizuri mambo ya leo, jamaa wote wanakuona unatabasamu. Na vilevile una mikono miwili, kama ukiweza kuchuma pesa itakuwa afadhali.' Na nilipomwaona mara ya pili, alikuja kwetu akiwa na tabasamu usoni. Alisema; 'ninakuja nyumbani kwa wakwe.' Naona sisi shirikisho la wanawake tukifanya jambo dogo, ama kumgusia kwa sentensi moja tu, tumekuwa mhimili wake."

    Kuanzia mwaka 2013, afya ya Chen Xiuhua ilianza kuwa nzuri kiasi, na kutokana na pendekezo lililotolewa na shirika la wanawake la eneo la Tongnan, ameanza kufuga sungura nyumbani. Kila aubuhi anaamka mapema sana na kushughulikia mambo madogo madogo hadi usiku wa manane, yote anayofikiria ni namna ya kufuga vizuri sungura wake.

    "Ninapoamka asubuhi, kwanza nawapa maziwa sungura kwa nusu saa, baadaye ninapika chakula, kuwafanyia sungura wa kike mzalishi, kuwalisha tena sungura, na kuanzia saa nne ninasafisha vyumba vya sungura. Ninalima na pia ninafuga kuku, bata na bata kukini 60 ama 70. Mbali na hayo napanda mahindi na Ixeris. Ninaporudi nyumbani usiku naendelea kushughulika na sungura."

    Ukubwa wa shamba la familia la ufugaji sungura la Chen Xiuhua umeongezeka siku hadi siku, kutoka sungura 6 tu hadi zaidi ya elfu 1 sasa. Na ni kutokana na Sungura hao, Chen ameweza kulipa zaidi ya nusu ya deni lake la kufanyiwa upasuaji.

    "Ndugu wa shirika la wanawake walitumia pesa zao wenyewe kunisaidia. Mmoja alisema: 'unaweza kushughulikia ufugaji, na alinisaidia kuanzisha shamba la ufugaji.' Mwanzoni nilifuga sungura wachache tu, baadaye kutokana na uungaji mkono na misaada yao, sasa ninaweza kupata pesa ambazo zinaweza kulipa gharama za kifamilia. Na hata naweza kupata karibu dola za kimarekani 500. Na kama nitashindwa kuwauza sungura wote, basi nitarudi nyumbani kwa wakwe zangu, shirikisho la wanawake, na hao watanunua wote tena kwa bei kubwa zaidi kuliko bei ya soko."

    Baada ya kuwa na maisha mapya, Chen Xiuhua akawa na wazo jipya, kuwasaidia wanawake wenye ugonjwa kama wake kushikamana. Kwenye hafla moja iliyoandaliwa na shirikisho la wanawake la Tongnan na kushirikishwa na wanawake, Chen Xiuhua amegundua kuwa wanawake wengi wanaougua kansa wamekata tamaa. Hivyo siku hiyo hiyo aliunda kikundi cha wanawake kujiokoa na kusaidiana. Hivi karibuni dada mmoja mwenye kansa aliyeko mjini Chongqing alikwenda nyumbani mwa Bibi Chen.

    "Alishtuka sana akasema: 'Wewe ni Chen Xiuhua? Mwenye kansa?!' Aliona nachapa kazi siku zote lakini kwa furaha kubwa, baadaye tulifanikiwa kumshawishi akafanyiwa upasuaji. Wakati alipofanyiwa upasuaji, sisi sote tulimhudumia. Sasa anaishi kwa amani siku nzima, tunawasiliana kwa simu takriban kila usiku."

    Wanakijiji wote wanamsifu Bibi Chen kuwa ni mkwe mwema, mama mwema na jirani mwema, vilevile ni mwanamke mkarimu sana kijijini. Wanawake wengine wakipatwa na shida zozote wanakwenda kuomba msaada kwa Bibi Chen, naye Chen huwasaidia kwa ukarimu mkubwa.

    "Dada Chen, nitawapatiaje kuku chanjo?"

    "Kwanza kabisa fuatilia wanavyokula. Kama wanaharisha, basi uwapigie simu, au kununua dawa uwape."

    "Nawalishe dawa kwa kiasi gani?"

    "Ufuate maelezo yanayoandikwa kwenye dawa, lakini uongeze kidogo."

    Machoni mwa jamaa wa Chen Xiuhua, yeye huingilia sana mambo ya watu wengine, lakini yeye mwenyewe husema, ukitaka wengine wakusaidie, basi uwasaidie vilevile. Na moyo huo bora wa kujiamini, na kujitegemea umebadili mtazamo wa maisha wa ndugu zake na hata mume wake.

    "Akili yake sina wasiwasi, na familia yetu inaonesha uso mpya, tuna furaha sasa. Shirikisho la wanawake wametusaidia na kutuunga mkono sana. Nimeguswa sana"

    Mwenyekiti wa shirikisho la eneo la Tongnan Dai Hongli anasema, Chen Xiuhua amekuwa mfano mzuri wa kuwahimiza wanawake kuwaunga mkono wanawake wenzao kuendeleza shughuli za kilimo na ufugaji, vilevile ametoa mchango wake kwa ajili ya kujitokeza familia bora nyingi zaidi na vijiji bora. Vilevile anaona juhudi zake zinaweza kuhimiza shirikisho lake kufanya kazi kwa kina na makini zaidi.

    "Mwenyekiti wa shirikisho la wanawake la mji alimwambia mkurugenzi wa shirikisho la wanawake la kijiji, ambaye aliongea na Chen Xiuhua kuwa: 'Xiuhua, Xiuhua, ……'naye Xiuhua alikabidhi fomu ya kugombea 'familia bora zaidi mjini Chongqing'. Nadhani kama wakurugenzi wote wa mashirikisho ya wanawake vijijini wanaweza kufanya kazi kama hii, basi hakuna jambo lolote lisiloweza kufanyika vizuri."

    Juu ya mpango wa shamba lake la familia la sungura katika siku za mbele, Chen Xiuhua anasema mpango huo sio tu unahusiana na shamba lake mwenyewe, bali pia unajumuisha wanawake wanaohitaji misaada.

    "Wanakijiji wengi wamefuata mfano wangu na kuanzisha mashamba ya kufuga sungura, na moja kati yao ukubwa wake ni sawa na langu. Mashamba mawili nyuma ya shamba langu, nayatembelea mara kwa mara kuangalia kama sungura wana matatizo yoyote, na ninawashauri pia. Kuhusu mpango wangu wenyewe, nimehesabu ubao wa sakafu, sehemu zote husika zimepangwa na hata zitapanuka. Kwani mume wangu na mtoto wangu wamerudi, nataka kupanua kidogo. Nasema tu kama mtu yeyote anahitaji msaada wangu, naweza kumpa sungura wangu bure, na kumsaidia awe tajiri zaidi."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako