• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mtandao wa Internet Enzi mpya kwa wanawake kuanzisha biashara

    (GMT+08:00) 2015-11-02 13:41:59

    Katika kipindi kilichopita, tulikufahamisha machache kuhusu Shamba la Familia ya Zhiqing lililoanzishwa na Bi. Zhang Tian, na jinsi lililovyoweza kukwamua familia hiyokiuchumi, lakini pia kuwa mfano kwa wanakijiji wenzake huko Tongnan, mji wa Chongqing, hapa China.

    Na katika kipindi cha leo, tunaelekea mjini Hangzhou, mashariki mwa China, mji ambao unasifiwa kuwa ni "maskani ya hariri". Miaka zaidi ya 200 KK, hariri kutoka Hangzhou iliuzwa ng'ambo kupitia "Njia maarufu ya Hariri" iliyounganisha mabara ya Asia, Ulaya na Afrika. Katika mji huo basi, tunakutana na Bi. Fan Xiaojing.

    Baada ya kumaliza kipindi cha asubuhi, Bibi Fan Xiaojing anaharakisha kwenda kwenye kampuni yake na kuanza kazi zake. Kampuni yake ilianzishwa mwezi Septemba mwaka jana, na inashughulika na uuzaji wa skafu (mitandio). Katika miaka ya hivi karibuni, njia ya kushirikisha "mtandao pamoja na shughuli za jadi" imeonesha nguvu kubwa ya uhai nchini China, na Hangzhou si kama tu ni kivutio cha utalii, bali pia imekuwa kivutio kwa waanzishaji shughuli za biashara kupitia mtandao wa internet. Kampuni ya Bibi Fan Xiaojing ni mojawapo.

    "Nawasiliana na mteja wa Shenzhen, anataka kuagiza skafu ya mitindo ya majira ya baridi, na anataka kuwasiliana nasi."

    Bibi Fan Xiaojing ni mwenyeji wa wilaya ya Tonglu mkoani Zhejiang, wakati angali mdogo, wazazi wake na mdogo wake wa kiume walikwenda nje ya Zhejiang kufanya kazi, na walimwacha na bibi yake. Ili kumtunza mjukuu wake, bibi Fan aliafanya kibarua katika kiwanda cha kofia cha huko, na kila wiki aliweza kupata Yuan 50 hivi. Kazi hiyo nzito ilifanya afya ya bibi kudorora, na Fan ambaye wakati huo alikuwa shule ya sekondari, alitaka kumpunguza bibi yake mzigo wa kumtunza kupitia kujiajiri.

    Kuna njia nyingi za kujiajiri, na kwa Fan, alipokuwa sekondari ya juu, alianza kufanya hivyo. Alinunu pipi kwa bei ya jumla, na kisha kuziuza rejareja shuleni. Alipoingia chuo kikuu, hamu yake ya kujiajiri ilikuwa inaongezeka, hivyo aliweka meza kwenye mtaa wenye watu wengi nyuma ya chuo na kuanza kuuza skafu. Baada ya mwezi mmoja, Fan aligundua kuwa bila kujali alifanya juhudi kubwa namna gani, aliweza kuuza skafu 20 tu kwa siku, akagundua kuwa ni kupitia mtandao tu, ndio biashara yake inaweza kupanuka.

    "Mwanzo nilipotaka kuweka meza, nilijua ni sehemu gani natakiwa kuweka, na idadi ya wapitaji ni muhimu sana kwangu. Hivi sasa mtandao ni maarufu, na idadi ya watu wanaotembelea mtandao ni kubwa zaidi kuliko barabarani, hivyo bila shaka nitakuwa na fursa nyingi zaidi kwenye mtandao wa internet, na watu wengi zaidi watajua skafu zangu. Kwa hiyo nikaanzisha biashara yangu kwenye mtandao wa internet, na watu wengi zaidi wakafahamu skafu zangu na kuniunga mkono."

    Naibu mkuu wa idara inayoshughulikia mambo ya miji na vijiji ya shirikisho la wanawake la Hangzhou Ye Qi amefahamisha kuwa, katika miaka mitano iliyopita, wengi wa wanachama wa shirikisho la wanaviwanda wanawake wengi wanashughulikia uchumi halisi, na wengi wao wanafanya biashara kupitia mtandao wa internet. Njia hiyo imetoa fursa nyingi kwa wanaviwanda wanawake, ambayo imepunguza tofauti kati ya wanaume na wanawake.

    "Uanzishaji shughuli kupitia mtandao wa internet ni muhimu kwa kuzoea uchumi, na wanawake wana fursas dhahiri katika jambo hilo, wanazingatia zaidi hisia za matumizi ya wateja na kuwasiliana nao. Wakati huohuo, wanawake wanapenda zaidi kazi zinazoshughulisha zaidi akili, na si mwili, hasa ni vizuri anaweza kukaa nyumbani, na mtandao wa internet ndio unakidhi mahitaji hayo. Tofauti na wanawake, wanaume wanaweza kwenda kila mahali kuanzisha shughuli, na wana mawasiliano ya kibinadamu zaidi kuliko wanawake. Lakini wanawake wanaweza kupata wateja wengi katika muda mfupi kupitia mtandao wa internet. Hivyo wanawake wanaanzisha shughuli zao kupita mtandao wa internet, hasa wanawake vijana, wana mustakabali mzuri."

    Ili kujifunza ujuzi wa kuendesha shughuli kupitia mtandao wa internet na kuongeza uzoefu wa kufanya biashara, Fan Xiaojing ameshiriki kwenye mafunzo ya mtandao wa internet na ufundi yaliyotolewa na shirikisho la wanawake mjini Hangzhou, ambapo amepata mafunzo kutoka kwa wanaviwanda wanawake, wafanyakazi wanawake wa sheria na walimu wanaosaidia wanawake kuanzisha shughuli, pia amewasiliana mara kwa mara na waanzishaji shughuli wanawake wengine kuhusu uzoefu wao katika kuanzisha shughuli. Kutokana na juhudi zake kubwa, ndani ya mwaka mmoja tu kampuni yao imepanuka kuajiri wafanyakazi 12, na biashara zao zimeenea kote nchini na hata Mashariki ya Kati.

    Mwanzo mdogo lakini kwa juhudi, biashara imepanuka, na hivi sasa Fan anafanya biashara katika maduka makubwa 6 ya biashara ya mtandao ikiwemo Alibaba na Taobao, na faida yake imefikia karibu Yuan laki 1.5 kila mwezi kutoka 3,000 ya mwanzoni, na skafu zao hata zinauzwa katika nchi za Mashariki ya Kati kama vile Saudi Arabia na UAE. Fan anasema,

    "Kama ningekuwa nimeweka meza tu, kamwe nisingeweza kuuza skafu zangu katika sehemu ya Mashariki ya Kati, watu wa nje ya nchi wasingejua kuwa nauza skafu, kwa hiyo nasema mtandao wa internet unanipa fursa nyingi, unanifanya nifahamu watu wengi na mambo mengi zaidi."

    Mfanyabiashara maarufu wa Hangzhou Zhao Wanli, ambaye pia ni mwalimu anayesaidia wanawake kuanzisha biashara zao amesema, katika zama inayosaidiwa na mtandao wa internet, kuanzisha shughuli kwa wanawake kumekuwa na mustakabali mzuri.

    "Mtandao wa internet unatupa fursa nyingi zaidi za kujiendeleza, ukilinganishwa na uchumi wa jadi wa kiviwanda, Uchumi wa sasa wa mawasiliano unafaa zaidi wanawake. Mfumo wa mtandao wa internet pamoja na wanawake hakika utatupa fursa nyingi zaidi."

    Wakati akianzisha biashara yake, Fan aliwahi kutunga mpango wa miaka mitatu, yaani katika mwaka wa kwanza, alitumai kuingia katika kituo cha uanzishaji shughuli cha chuo kikuu; katika mwaka wa pili, kuanzisha kampuni yake yenyewe; na katika mwaka wa tatu, anaweza kuwa na gari lake. Sasa umeingia mwaka wa tatu baada ya kuanzisha shughuli, ambapo atatimiza lengo lake, ana matarajio makubwa zaidi kwa kampuni yake.

    "Nyuma ya kadi ya kila mtu wa kampuni yetu kuna sentensi moja isemayo lengo letu ni kuifanya bahari yetu ya kusini kuwa chapa maarufu inayouzwa nje kutoka China. Hii ni lengo letu kuu, natumai tutatimiza lengo hilo."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako