• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mpango wa 13 wa miaka mitano wa China watoa fursa kwa dunia

    (GMT+08:00) 2015-11-11 11:31:28

    bendera ya taifa la China ikipeperushwa juu ya Ukumbi Mkuu wa Mikutano ya Umma mjini Beijing, China

     

    Ili kutoa mipango kuhusu miradi mikubwa ya kiujenzi, usambazaji wa nguvu za uzalishaji na uhusiano muhimu wa urari wa uchumi wa kitaifa, kuanzia mwaka 1953, serikali ya China ilianza kutoa "mpango wa miaka mitano" unaoainisha malengo na mwelekeo wa maendeleo katika miaka mitano inayofuata. Huu ni mwaka wa kumalizia mpango wa miaka mitano ya kuanzia mwaka 2010 hadi 2015. Kikao cha tano cha wajumbe wote cha Kamati Kuu ya 18 ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC kilichomalizika mwishoni mwa mwezi Oktoba kilijadili na kupitisha "pendekezo la kutunga mpango wa 13 wa miaka mitano wa maendeleo ya uchumi na jamii" na kubainisha maeneo yatakayotiliwa mkazo kimaendeleo katika miaka mitano ijayo nchini China.

    Taarifa iliyotolewa kwenye Kikao hicho imesema miaka mitano ijayo ni kipindi muhimu kitakachofanikisha lengo la kujenga jamii yenye ustawi mzuri wa pande zote nchini China, na "mpango wa miaka mitano ijayo" unapaswa kutungwa kwa ajili ya kutimiza lengo hilo. Taarifa hiyo pia imetoa malengo mapya katika kazi za kujenga jamii yenye ustawi wa pande zote, ikiwemo uchumi kukua kwa kasi ya kati na hadi kubwa; pato la taifa la China na kipato cha mtu mmoja mmoja kuongezeka kwa mara 2 kuliko mwaka 2010 kwenye msingi wa kuhimiza maendeleo yenye uwiano, jumuishi na endelevu; sekta za kiviwanda kuinuka hadi kwenye ngazi ya kati na ya juu, mchango unaotolewa na matumizi kwa ukuaji wa uchumi kuongezeka kidhahiri, na ukuaji wa mji kuimarishwa zaidi. Akizungumzia kuhusu malengo ya maendeleo ya uchumi katika miaka mitano ijayo, naibu mkuu wa taasisi ya utafiti wa uchumi wa jumla iliyo chini ya Kamati ya Maendeleo na Mageuzi ya China Ma Xiaohe anasema,

    "Taarifa inasema uchumi unapaswa kukua kwa kasi ya kati na kubwa, hii inamaanisha kuwa kasi ya ukuaji haipaswi kuwa ndogo, kama ni ndogo, itatuzuia kutimiza lengo la kujenga jamii yenye ustawi wa pande zote. Kasi hiyo hairuhusiwi kuwa chini ya asilimia 6.5, ama sivyo malengo kuhusu kipato cha mtu mmoja mmoja, ajira na hata huduma za umma za serikali hayatatimia, na kasi ya kati na kubwa inapaswa kuwa asilimia 6.5 hadi 7."

    eneo la biashara CBD jijini Beijing

    Katika miaka zaidi ya 30 iliyopita, uchumi wa China ulikua kwa kasi, hali ambayo siyo tu imeendeleza nchi hiyo, bali pia imetoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya uchumi wa dunia. Hata hivyo katika miaka ya hivi karibuni, muundo wa jadi wa maendeleo wa China ulikumbwa na vikwazo na changamoto za maliasili, mazingira na ardhi, na ili kukabiliana na matatizo hayo, China ilianza kutafuta marekebisho ya muundo wa kiuchumi. Wakati huohuo, kasi ya ukuaji wa uchumi ilianza kupungua, na uchumi wa China ukaingia kwenye hali mpya ya kawaida ya "ukuaji wa wastani wa kasi, marekebisho ya muundo, injini mpya na changamoto nyingi". Mtafiti wa idara ya utafiti wa uchumi wa dunia ya Taasisi ya Utafiti wa Uhusiano wa Kimataifa wa Kisasa ya China Chen Fengying anasema,

    "Naona injini za maendeleo ya uchumi wa China zinabadilika. 'Mpango wa 13 wa miaka mitano' unapaswa kuonesha mabadiliko, na jinsi ya kuzoea mabadiliko hayo, na pia sera zinatakiwa kutungwa kwa kuendana na 'hali mpya ya kawaida'."

    Hivi sasa, uchumi wa China uko kwenye kipindi cha kupunguza kasi ya ukuaji, kuufanyia marekebisho muundo na kusubiri kuonekana kwa ufanisi wa sera zilizotangazwa hivi kairbuni. Naibu mkuu wa taasisi ya utafiti wa uchumi wa jumla iliyo chini ya Kamati ya Maendeleo na Mageuzi ya China Ma Xiaohe anaona kuwa kipaumbele cha kwanza cha sasa kwa uchumi wa China ni kufanya mwendelezo mzuri wa muundo wa zamani wa maendeleo na maendeleo mapya yanayopatikana katika "hali mpya ya kawaida".

    "Katika siku zilizopita, injini ya uchumi ilitokana na maendeleo ya sekta za ngazi ya chini na kati zikiwemo sekta ya kemikali nzito na zile zinazotoa uchafu mwingi. Katika hatua zijazo, tutaendeleza zaidi sekta za usindikaji, zenye thamani kubwa ya nyongeza, teknolojia ya hali ya juu na zisizotoa uchafu mwingi. Lakini ugumu ni kuwa sekta zilizo nyuma, zinazotumia nishati nyingi na kutoa uchafuzi mwingi zinaondolewa, na gharama za sekta za ngazi ya chini zinaongezeka na kuhamishwa kwa nje, lakini sekta mpya za teknolojia ya juu zinaongezeka taratibu, hivyo juhudi zinatakiwa ili kufanya uratibu na kuhimiza mwendelezo mzuri kati yao."

    Mpango wa 13 wa miaka mitano ni mpango wa kwanza wa miaka mitano baada ya uchumi wa China kuingia kwenye "hali mpya ya kawaida", na ili kuzoea "hali mpya ya kawaida", kikao cha tano cha wajumbe wote wa Kamati Kuu ya CPC kilitoa mapendekezo matano kuhusu maendeleo, ambayo ni uvumbuzi, uratibu, kijani, ufunguaji mlango na mabadilishano. Naibu mkurugenzi wa ofisi ya kikundi cha Kamati Kuu kuhusu masuala ya fedha Yang Weimin anasema,

    "Mapendekezo hayo matano ni mageuzi ya kina katika maendeleo yetu, na pia yataamua jinsi tutakavyohimiza maendeleo baada ya kutimiza lengo la kujenga jamii yenye ustawi mzuri wa pande zote. Ni kweli tunajitahidi kujenga jamii yenye ustawi, lakini kama masuala yakijitokeza katika mchakato huo, basi hatuna budi kuyashughulikia baadaye, hili ni jambo lisiloweza kukubalika."

    Baada ya mkutano mkuu wa 18 wa CPC kufanyika mwaka 2012, kuimarisha mageuzi na kuinua kiwango cha uchumi unaofungua mlango vimekuwa mambo mawili muhimu. Profesa Liu Gang wa Chuo Kikuu cha Nankai mjini Tianjin anasema,

    "Pendekezo lililotolewa na Kikao cha tano cha Kamati Kuu ya 18 ya CPC limezungumzia sana uchumi unaofungua mlango. Katika siku zilizopita, ni kufungua mlango kwa nchi za nje tu, lakini sasa kuna tofauti, kwa mfano eneo la majaribio la biashara huria la Tianjian litajengwa kuwa eneo muhimu la kiuchumi ili kusaidia makampuni ya China kushiriki kwenye ushindani wa kimataifa, na kutoa mtaji na teknolojia kwa nje. Halafu utaratibu huo utaenezwa kote nchini ili kutimiza lengo la kuhimiza mageuzi na maendeleo ya uchumi wa China."

    Watu wengi wanaona kuwa mageuzi na ufunguaji mlango wa China katika "hali mpya ya kawaida" vitatoa fursa nyingi za maendeleo kwa dunia. Mwenyekiti wa Shirikisho la Makampuni Madogo na Yenye Ukubwa wa Kati la Ujerumani Winfried Bostelmanna ndiye anayeshikilia msimamo huo.

    "China ina bahati nzuri, kwani uchumi wake bado unaongezeka kwa kasi kubwa. Lakini kwetu nchini Ujerumani, kasi ya ongezeko ni asilimia 1.5 hadi 1.7 tu kwa mwaka, kwa hiyo ingawa uchumi wa China ulikua kwa asilimia 6.9 katika robo ya tatu ya mwaka huu, lakini hii ni hali mpya ya kawaida. Kwa makampuni ya Ujerumani, soko la China lina fursa nyingi, na tunafurahi kwa kuona uchumi wa uchumi wa China una mwelekeo wenye nguvu kama huo."

    Mwenyekiti wa Shirikisho la M&A la Ujerumani Profesa Kai Lucks anaona kuwa Taarifa iliyotolewa kwenye Kikao cha tano cha Kamati Kuu ya CPC inasisitiza kushikilia maendeleo yanayofungua mlango, kuendeleza uchumi unaofungua mlango wenye ngazi ya juu zaidi, kuongeza mshahara wa wafanyakazi wa teknolojia na ufundi, na kuzingatia kuongeza sifa ya wananchi, mambo hayo yatatoa fursa kwa makampuni ya Ujerumani kujihusisha na maendeleo ya China. Profesa Lucks anasema,

    "Makampuni mengi ya Ujerumani yanatafuta fursa za maendeleo kimataifa, na China ni soko kubwa duniani katika sekta nyingi, hii imetoa fursa kwa makampuni yetu ya Ujerumani. Pia nchini China wapo wafanyakazi wengi wa teknolojia na ufundi wenye sifa nzuri, ambao wamepewa mafunzo mazuri na kufanya kazi kwa bidii."

    Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa kwenye Kikao hicho, kuanzisha hali mpya ya ufunguaji mlango kwa nje kunatakiwa kuongeza mambo mapya, ambayo ni ufunguaji mlango, kuinua kiwango cha ufunguaji mlango kwa nje na kukamilisha sekta zinazofunguliwa kwa nje, kuhimiza ufunguaji mlango ndani ya nchi na kwa nje, na kuanzisha mfumo mpya wa ufunguaji mlango kwa nje na kujenga mazingira ya kibiashara yanayorahishwa na kufuata utawala wa sheria na mwelekeo wa kimataifa. Mwanauchumi mkuu wa idara ya makadirio ya uchumi katika Kituo cha Habari cha China Zhu Baoliang anasema faida kubwa inayotokana na ufunguaji mlango kwa nje ni mafanikio kwa pande zote.

    "Kwa upande mmoja, tutaendelea kufungua baadhi ya sekta zetu kwa nje, na pia kufanya ushirikiano na nchi za nje katika sekta kadhaa ili sekta hizo ziweze kufanya kazi katika nchi za kigeni na kusaidia kuchangia uuzaji wa bidhaa za China nje na uwekezaji nje ya nchi. Kwa upande mwingine, tutaendelea kuingiza teknolojia na mashine za kisasa nchini China, ili kuinua kiwango cha teknolojia cha China."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako