• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa kilele kati ya Umoja wa Ulaya na Afrika watangaza mpango wa kukabiliana suala la wakimbizi

    (GMT+08:00) 2015-11-13 18:44:54

    Mkutano wa kilele kati ya Umoja wa Ulaya na Afrika kuhusu suala la wakimbizi ulifanyika juzi na jana mjini Valletta, Malta, ambapo viongozi wa Ulaya na Afrika wameafikiana kuhusu kuimarisha ushirikiano na kutatua msukosuko wa wakimbizi, na pia wametangaza azimio la kisiasa na mpango wa utekelezaji.

    Mkutano huo unachukuliwa na Umoja wa Ulaya kuwa ni hatua muhimu ya kukomesha wimbi la wakimbizi kuanzia nchi wanazotoka, na kutimiza matakwa yao matano yakiwemo kuhamasisha uhamiaji halali, kulinda maslahi ya wakimbizi, kupambana na ulanguzi wa binadamu, kuhakikisha wakimbizi wanarudishwa bila matatizo na kuisiaidia Afrika kujenga amani, utulivu na maendeleo.

    Katika mkutano na waandishi wa habari, mwenyekiti wa baraza la Ulaya Bw. Donald Tusk ameeleza mpango wa utekelezaji, yaani kujenga mpango wa maendeleo na uhifadhi wa kikanda katika Afrika ya Kaskazini, kuanzisha kundi la uchunguzi la pamoja la kupambana na ulanguzi wa binadamu, kuwaalika maofisa wa idara za uhamiaji za nchi za Afrika kwenda Ulaya kuwatambua na kuwarudisha wakimbizi, na kuongeza idadi ya wanafunzi na watafiti wanaopewa udhamini wa Umoja wa Ulaya. Bw. Tusk amesema msukosuko wa wakimbizi unahitaji Umoja wa Ulaya na nchi za Afrika kushirikiana kukabiliana nao.

    "changamoto ya msukosuko wa wakimbizi inatuhitaji tushirikiane. Hakuna yeyote anayeweza kutatua suala hili peke yake, hii ndio sababu kuu ya kufanya mkutano huo. "

    Ingawa msimamo wa Ulaya na Afrika unaonekana ni sawa, lakini zina maoni ya tofauti katika kuweka hatua halisi. Rais Macky Sall wa Senegal amesema mambo yaliyomo kwenye mpango huo yanatarajiwa kuboreshwa, lakini pia amesisitiza kuwa, pande mbili hakika zitatatua suala hilo kupitia ushirikiano.

    "naona mambo yaliyomo kwenye mpango huo yanatarajiwa kukamilishwa, lakini jambo muhimu zaidi kwa sasa ni utekelezaji wa mpango huo. Ingawa Ulaya na Afrika zina msimamo wa sawa, lakini zinapotatua suala la wakimbizi huenda zikafuata njia tofauti. Zikishirikiana, hakika zitatatua suala la ulanguzi wa binadamu na uhamiaji haramu. "

    Siku hiyo Umoja wa Ulaya pia umeidhinisha kuanzisha mfuko wa dhamana kwa ajili ya nchi za Afrika kutatua suala la wakimbizi. Umoja wa Ulaya utatenga Euro bilioni 1.8 kutoka kwenye bajeti yake na mfuko wa maendeleo ya Ulaya kwenye mfuko huo wa dhamana, na pia utazihamasisha nchi 28 wanachama kuchangia mfuko huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako