• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mambo sita kuhusu mustakbali wa uchumi wa China katika kipindi cha mpango wa 13 wa maendeleo ya miaka mitano

    (GMT+08:00) 2015-11-18 10:07:30

    Mpango wa 13 wa maendeleo ya miaka mitano wa China uliotolewa na kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China umethibitisha kuwa kipindi cha mpango huo ni kipindi muhimu cha kukalimisha ujenzi wa jamii yenye maisha bora. Kumekuwa na maswali kuwa, China ikiwa inakabiliwa na changamoto mbalimbali, itakuwa na mwelekeo gani wa maendeleo, na itatatua vipi matatizo hayo ili kujiendeleza? Katika kipindi hicho cha uchumi na maendeleo, tutaeleza mambo sita kuhusu mpango huo.

    **

    Moja ya mambo yaliyotajwa kwenye mpango huo ni ongezeko la uchumi, ambalo limetajwa kuwa la kasi ya kati, lakini je kasi hiyo ya ongezeko ni ya namna gani? Mkurugenzi wa Taasisi ya utafiti wa hali nchini China katika Chuo Kikuu cha Tsinghua Prof. Hu Angang alisema uchumi wa China utaingia kipindi kipya cha maendeleo, ingawa ongezeko la uchumi litapungua, lakini ongezeko la asilimia 7 bado ni kiwango cha juu. Mkurugenzi wa idara ya uchumi wa jumla katika kituo cha utafiti wa maendeleo cha Baraza la serikali la China Bw. Yu Bin alisema, kama ongezeko la uchumi la mwaka huu litafikia asilimia 7, basi wastani wa ongezeko la uchumi wa China katika kipindi cha mpango wa 12 wa maendeleo ya miaka mitano utakuwa asilimia 7.8. China ikitaka kutimiza lengo la kuongeza pato la taifa GDP kwa maradufu kuliko mwaka 2010 ifikapo mwaka 2020, wastani wa ongezeko la uchumi katika kipindi cha mpango wa 13 wa miaka mitano utatakiwa kufikia asilimia 6.5. Aliongeza kuwa katika hali mpya, ingawa China haiwezi kutafuta ongezeko kubwa lisiloweza kutimizwa, lakini uchumi ukipungua kwa kiasi kikubwa ndani ya muda mfupi, ni vigumu kwa China kubadilisha muundo wa uchumi wake.

    Mkurugenzi wa kitivo cha uchumi cha Chuo cha utawala cha China Prof. Zhang Zhanbin ana imani kuhusu uchumi wa China kudumisha ongezeko la asilimia 7 katika kipindi cha mpango wa 13 wa miaka mitano, akisema kuwa hivi sasa ongezeko la uchumi linafufuka, muundo wa uchumi unaboreshwa hatua kwa hatua, mambo hayo yote yanaonesha kuwa uchumi wa China utapata maendeleo katika miaka mitano ijayo.

    **

    Jambo lingine lililotajwa kwenye mpango huo ni injini mpya ya uchumi wa China. Hivi karibuni eneo la Putuo mjini Shanghai lilitoa sera mbalimbali za kuhimiza uvumbuzi, zikiwemo kuanzisha mfuko wa kuzihimiza idara za uwekezaji na mitaji ya kijamii kuwekeza makampuni ya sayansi na teknolojia, na kuyasaidia makampuni madogo na ya ukubwa wa kati kununua huduma za sayansi na teknolojia. Mkuu wa eneo la Putuo Bw. Cheng Xiangmin alisema uvumbuzi ni injini muhimu ya maendeleo, na eneo la Putuo litaendelea kutoa huduma bora na kuweka mazingira mazuri kwa makampuni kufanya uvumbuzi.

    Naibu mkurugenzi wa taasisi ya utafiti wa uchumi wa jumla ya kamati ya maendeleo na mageuzi ya China Bw. Chen Dongqi alisema kwa sasa matumizi ya fedha katika shughuli za kuwatunza wazee, afya, utalii na mauzo kupitia mtandao wa Internet yanapata maendeleo makubwa, na yamesukuma mbele maendeleo ya uchumi kwa kiasi kikubwa. Maendeleo ya miji nchini China bado yako nyuma kuliko nchi zilizoendelea, hivyo uchumi wa China bado una uwezekano mkubwa wa kupata maendeleo zaidi. Aliongeza kuwa katika kipindi cha mpango wa 13 wa miaka mitano, matumizi ya fedha na uvumbuzi zinatazamiwa kuwa injini mbili kuu za kuhimiza maendeleo endelevu nchini China.

    **

    Lingine lililofuatiliwa ni kwamba China itahitaji kuchukua hatua ngapi ili kutimiza lengo la kuwa na uzalishaji viwandani wa kiwango cha juu.Mwezi Julai mwaka huu, kampuni ya treni za umeme ya Zhuzhou ya kampuni ya CRRC ilimaliza utengenezaji wa treni zenye injini nyingi zinazoagizwa na Macedonia, hii ni mara ya kwanza kwa treni za aina hiyo zilizotengenezwa na China kuingia kwenye soko la Ulaya. Mkurugenzi wa kamati ya wataalamu ya kampuni hii Bw. Liu Youmei amesema makampuni ya China yakitaka kuingia kwenye soko la kimataifa, yanahitaji kuwa na uwezo mkubwa wa kufanya uvumbuzi.

    Mkutano wa kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China umeamua kuwa China itaanzisha mfumo mpya wa viwanda, kuharakisha ujenzi wa nchi yenye uwezo mkubwa wa uzalishaji viwandani, kutekeleza mradi wa kuimarisha msingi wa viwanda, kuanzisha shughuli mbalimbali za kimkakati, na kuharakisha maendeleo ya sekta ya huduma. Mkuu wa taasisi ya utafiti wa mageuzi na maendeleo ya Hainan Bw. Chi Fulin anaona kuwa katika kipindi cha mpango wa 13 wa maendeleo wa miaka mitano, China itaongeza kasi ya sekta ya huduma, na kutilia maanani uhusiano kati ya sekta za huduma, kilimo na viwanda.

    Naibu mkuu wa taasisi ya tafiti wa uchumi wa jumla ya kamati ya maendeleo na mageuzi ya China Bw. Ma Xiaohe alisema katika siku zijazo kazi muhimu ya mageuzi ya sekta ya uzalishaji viwandani itakuwa ni kuimarisha utengenezaji wa bidhaa ya teknolojia ya hali ya juu, kufanya uvumbuzi katika shughuli muhimu, kuachana na mbinu za uzalishaji zilizopitwa na wakati, na kuunga mkono shughuli mpya za kimkakati.

    **

    Vilevile kumekuwa na swali kuhusu ni vipi kazi ngumu za mageuzi zitafanyika. Katika kipindi cha mpango wa 13 wa miaka mitano, China itakuwa na kazi mbalimbali za mageuzi, na kazi nyingi ni ngumu. Kama China itasukuma mbele mageuzi, itatatua suala la kimuundo, na kutoa uhakikisho kwa ujenzi wa jamii yenye maisha bora.

    Mkutano wa kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China umesema China itaimarisha mageuzi kwa mfumo wa utawala na usimamizi, kukamilisha utaratibu wa usimamizi wa mali za kiserikali, kuanzisha mfumo wa kisasa wa fedha na kodi, na kuboresha utaratibu wa usimamizi wa mambo ya fedha unaoendana na maendeleo ya soko la fedha.

    Kuwa na imani na kuhimiza utekelezaji wa sera mbalimbali ni muhimu katika kufanikisha kazi ngumu za mageuzi. Naibu mkuu wa idara ya habari ya kituo cha mawasiliano ya kiuchumi ya kimataifa Bw. Wang Jun alisema, serikali ya China inatakiwa kutoa mipango muhimu ya mageuzi, kutekeleza mipango kwa makini, kuondoa vizuizi na kuongeza ufanisi wa utekelezaji wa mipango hiyo.

    **

    Maendeleo mapya ya maeneo mbalimbali pia yalifuatiliwa kuwa yatapangwa vipi. Hivi karibuni meneja mkuu wa kampuni ya ufugaji ya Mengyang Bw. Yan Shuchun alifuatilia sana ujenzi wa mradi wa vielelezo wa ufugaji usio na uchafuzi wenye ukubwa wa hekta 667. Kutokana na maendeleo ya shughuli za kupanda mazao kwa wingi na kutengeneza bidhaa za mifugo kwa kufuata vigezo vya uzalishaji, mauzo ya kampuni hii kwa mwaka jana yalizidi yuan bilioni 1.2, na mwaka huu yanakadiriwa kuzidi yuan bilioni 2. Kuhifadhi mazingira na kutafuta maendeleo endelevu ni maoni ya pamoja ya maeneo yenye rasilimali nyingi za ufugaji katika sehemu za kati na magharibi mwa China.

    Mwaka huu China imeharakisha kuendeleza maeneo mbalimbali, na sera muhimu husika zimetolewa. kutokana na utekelezaji wa mkakati wa kuendeleza maeneo manne ya mashariki, kati, magharibi na kaskazini mashariki nchini China, na mkakati wa kuendeleza kanda tatu za kiuchumi zikiwemo ukanda wa kiuchumi wa njia ya hariri ya karne ya 21, ukanda wa miji ya Beijing na Tianjin na mkoa wa Hebei, na ukanda wa kiuchumi kando ya mto Changjiang, maeneo mbalimbali yanapata maendeleo yenye uwiano zaidi, na uchumi wa baadhi ya mikoa ya kati na ya magharibi unapata ongezeko kubwa zaidi kuliko mikoa iliyoko mashariki mwa China.

    Bw. Wang Jun alisema China inatakiwa kuondoa vikwazo vya kimfumo ili kusukuma mbele maendeleo ya uchumi kwa uwiano, kuhimiza mawasiliano ya rasilimali, na kuinua uwezo wa uzalishaji kupitia mageuzi na uvumbuzi.

    **

    Hata hivyo kumekuwa na swali lingine kuhusu maendeleo ya kazi ya ya kuinua kiwango cha kufungua mlango, Mkutano wa kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China umesisitiza kuwa ufunguaji mlango unatakiwa kuendana na mwelekeo wa uchumi wa China unaoungana zaidi na uchumi wa dunia, kufuata mkakati wa kunufaishana na kupata mafanikio kwa pamoja, kuendeleza uchumi ulio wazi kwa kiwango cha juu zaidi, kushiriki zaidi kwenye mambo ya kiuchumi duniani, kuinua uwezo wa kutoa sauti kuhusu mambo hayo, na kuanzisha uhusiano na nchi nyingi zaidi.

    Bw. Zhang Zhanbin alisema China itatilia maanani ujenzi wa ukanda wa njia ya hariri na njia ya hariri ya baharini ya karne 21, kuongeza ushirikiano na nchi za nje katika uzalishaji wa nishati na utengenezaji wa mashine, na kuanzisha utaratibu mpya wa ufunguaji mlango katika pande zote.

    Mtafiti wa taasisi ya wizara ya biashara ya China Bw. Huo Jianguo anaona kuwa kama China ikitaka kuanzisha utaratibu mpya wa ufunguaji mlango, inatakiwa kuweka mazingira ya kibiashara ambayo yanasimamiwa kwa mujibu wa sheria, kushirikiana vizuri na dunia, na ni rahisi kwa wafanyabiashara kufanya shughuli zao, na kupanua ufunguaji mlango katika sekta ya huduma hatua kwa hatua.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako