• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa China na Afrika Kusini kuendesha kwa pamoja mkutano wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika

    (GMT+08:00) 2015-11-26 09:50:06

    Naibu waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Zhang Ming amesema, rais Xi Jinping wa China atahudhuria na kutoa hotuba kwenye ufunguzi wa mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika huko Johannesburg, pia ataendesha mkutano wa wajumbe wote wa mkutano huo pamoja na mwenzake wa Afrika Kusini rais Jacob Zuma.

    Kwenye mkutano na waandishi wa habari, Bw. Zhang amesema rais Xi kwanza atafanya ziara nchini Zimbabwe tarehe 1 hadi 2 Desemba, ambako atafanya mazungumzo na rais Robert Mugabe na kushuhudia kusainiwa kwa nyaraka za ushirikiano katika sekta mbalimbali. Bw. Zhang amesema hii ni mara ya kwanza kwa rais Xi kuzuru Zimbabwe. Baadaye tarehe 2 hadi 3, rais Xi atafanya ziara nchini Afrika Kusini, na kufanya mazungumzo na rais Zuma, ambapo nchi hizo mbili pia zitasaini nyaraka mbalimbali za ushirikiano.

    Kamati kati ya wizara nchini Afrika Kusini imesema, nchi hiyo iko tayari kuandaa mkutano wa wakuu wa ushirikiano kati ya China na Afrika. Mkurugenzi wa kikanda wa shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo ya viwanda, UNIDO Jean Bakole amesema, mkutano huo unatarajiwa kujadili njia za kuimarisha uhusiano wa kiuchumi kati ya China na Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako