• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hakuna taarifa kwamba Marekani inakabiliwa na tishio la kigaidi

    (GMT+08:00) 2015-11-26 10:42:01
    Rais Barack Obama wa Marekani amesema hakuna taarifa za kijasusi za kuaminika zinazoonesha kuwa magaidi wanapanga kuishambulia Marekani, na serikali ya Marekani inachukua hatua zote ili kuhakikisha usalama wa nchi.

    Mapumziko ya Siku ya Shukurani yameanza leo nchini Marekani, na kundi la IS hivi karibuni lilitangaza mara kadhaa kuwa litashambulia sehemu nyingi zikiwemo Washington na New York, na hata kimetishia kuchoma Ikulu ya Marekani. Rais Obama jana aliitisha mkutano wa kujadili hali ya usalama nchini Marekani baada ya tukio la mashambulizi ya kigaidi mjini Paris.

    Habari nyingine zinasema waziri wa mambo ya ndani ya Ufaransa Bw. Bernard Cazeneuve jana alitangaza kuwa, Ufaransa itaweka askari polisi 11,000 ili kuhakikisha usalama wa mkutano kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa utakaofunguliwa mwisho wa mwezi huu huko Paris. Amesema askari polisi 8,000 watashughulikia ukaguzi wa mipaka nchini humo, na wengine 2800 watashughulikia usalama wa eneo la mkutano huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako