• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNCTAD lapendekeza mwongozo mpya wa kutokomeza umasikini vijijini kwenye nchi zenye maendeleo madogo duniani

    (GMT+08:00) 2015-11-26 20:26:29

    Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo UNCTA imesisitiza umuhimu wa kuongeza uwekezaji wa miundo mbinu na uzalishaji wa kilimo wakati zikikuzwa shughuli zisizo za kilimo katika nchi zenye maendeleo madogo duniani.

    Kwenye ripoti hiyo iitwayo Nchi zenye Maendeleo Madogo Duniani ya mwaka 2015: Kufanya mageuzi ya uchumi wa vijijini, shirika hilo limependekeza mwongozo mpya wa kukabiliana na umasikini vijijini na kukosekana kwa maendeleo katika mageuzi ya vijijini, mambo ambayo ndio chanzo cha uhamiaji ndani na kutoka nchi zenye maendeleo madogo duniani.

    Akiongea kwenye uzinduzi wa ripoti hiyo Katibu Mkuu wa UNCTAD Mukhisa Kituyi amesema katika nchi nyingi zenye maendeleo madogo, uhamiaji unasababishwa na umasikini vijijini, ikionesha ukosefu wa fursa za uchumi za kujipatia angalau mapato ya chini ya kutosha. Amesisitiza kuwa utatuzi pekee wa msukosuko wa uhamiaji ni kutokomeza umasikini vijijini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako