• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya ina matumaini ya kutwaa kombe la Cecafa Senior Challenge

    (GMT+08:00) 2015-11-27 09:52:21

    Rais wa shirikisho la soka nchini Kenya FKF Sam Nyamweya amesema ana matumani kuwa Kenya italitwaa kombe la Cecafa Senior Challenge Cup linaloendelea nchini Ethiopia.

    Nyamweya anayasema hayo licha ya kuwa timu ya Kenya Harambe stars ilitoka sare ya bao 1-1 na Burundi.

    Alisema Ushindi wao dhidi ya Uganda baada ya miaka 11 ilikuwa ni dhihirisho tosha kwamba watatia fora katika makala ya 2015.

    Michuano ya CECAFA CHALENJI CUP 2015 itaendelea leo ijumaa kwa michezo kadhaa, Rwanda wataikabili somalia, vibonde Zanzibar Heroes watakuwa viwanjani dhidi ya Kenya.

    Sudan Kusini watawakabili Malawi na Djibouti itachuana na Sudan.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako