• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Saudi Arabia kuhimiza wapinzani wa Syria kushiriki kwenye mazungumzo ya amani

    (GMT+08:00) 2015-11-27 10:02:03

    Waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia Bw. Adel al-Jubeir amesema, Saudi Arabia itaitisha mkutano utakaoshirikisha makundi mbalimbali ya upinzani nchini Syria na kuratibu misimamo yao ili ishabihiane na kushiriki kwa pamoja kwenye mazungumzo kati yao na serikali ya Syria.

    Bw. Jubeir pia amesisitiza kuwa Saudi Arabia haitawasiliana na wapinzani wa Syria waliowekwa kwenye orodha ya makundi ya kigaidi.

    Tarehe 14 mwezi huu mkutano wa pili wa mawaziri wa mambo ya nje kuhusu mgogoro wa Syria ulifanyika huko Vienna, ambapo maoni ya pamoja yalifikiwa kuhusu ajenda ya mchakato wa kisiasa wa Syria, na kwamba serikali ya Syria na wapinzani wanatakiwa kuunda serikali ya mpito ndani ya miezi 6 kupitia mazungumzo, na kufanya uchaguzi mkuu ndani ya miezi 18.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako