• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hisia za wachina kuhusu kuondolewa kwa sera ya mtoto mmoja

    (GMT+08:00) 2016-01-05 08:22:10

    Hivi karibuni serikali ya China iliamua kufuta sheria iliyodumu kwa zaidi ya miongo mitatu iliyokuwa ikizitaka familia za nchi hii kutozaa zaidi ya mtoto mmoja. Wanandoa sasa wanaweza kuzaa watoto wawili, hatua hii ikiwa imechukuliwa ili kuepuka mwanya wa ukosefu wa nguvu kazi kwani watu wengi wanaendelea kuzeeka. Sheria hii mpya hata hivyo imepokelewa kwa hisia tofauti na raia wa China.

    Mzee Xin mwenye umri wa miaka 71 alifunga ndoa mwaka 1969 baada ya kustaafu kutoka jeshi. Wakati ule, sera ya familia moja yenye mtoto mmoja bado haikutekelezwa. Lakini mzee huyo alikuwa anafikiri watoto wengi wanaweza kushusha kiwango cha maisha, hivyo alizaa watoto wawili.

    Lakini miaka kumi badaaye mwaka wa 1979 serikali iliweka sera ya kuzaa mtoto mmoja tu kwa kila wanandoa ili kuzuia ongezeko la watu kupita kiasi isichoweza kumudu. Na sasa, sera ya kuwa na watoto wawili imetolewa, na yeye ni babu. Alisema: "Mimi na mke wangu sitaki wajukuu wengi, kwa sababu watoto wengi ni mzigo kwa familia, ambao utapunguza sifa ya maisha. Huyu ni mtoto wa pili wa mwanangu. Mwanangu anataka mtoto wa pili, anasema mmoja atajisikia upweke. Lakini mimi na mke wangu hatupingi wala hatumungi mkono. Upinzani wetu pia haufanyi kazi."

    Kwa watoto wengi waliozaliwa baada ya mwaka wa 1979 hawana ndugu wala dada. Wamepata upendo wa wazazi wengi kwani wao ni watoto wa pekee lakini pia wamekosa uzoefu wa kucheza na mtoto mwenza kwenye familia.

    Mu Zi aliyezaliwa baada ya miaka 80 kutoka familia yenye mtoto mmoja. Alisema: "Nilipokuwa utotoni, nilikuwa najisikia upwekee. Lakini katika jamii ya sasa, ukitaka kuwatunza watoto wawili, utashindwa kulipia gharama ya juu. Kwa mfano, ukiwa na mtoto mmoja, unaweza kumnunulia vitu vizuri zaidi, lakini ukiwa na watoto wawili utafikiria gharama unayolipa."

    Lakini kulingana na maoni ya wengi, hata bila kuwepo na sera ya kuzaa mtoto mmoja bado wanaona kwamba tayari maisha ni magumu na zaidi ya mtoto mmoja ni mzigo mkubwa kwao. Bali na kuwa serikali inatoa elimu ya msingi na sehemu ya sekondari bila malipo, lakini gharama za matibabu na nyumba ziko juu sana.

    Mwalimu wa shule ya msingi Bibi Sun anasema idadi ya watoto unaozaa sio hoja, umuhimu ni kuwaelimisha. Alisema: "Kuwalea watoto si jambo gumu, lakini kuelimisha watoto ni kazi ngumu sana. Unatakiwa kuwafundisha watoto misimamo sahihi kuhusu dunia, jamii na maisha, kuwasaidia kutunga mpango kuhusu siku za mbele. Kwa hivyo wazazi wanatakiwa kufikiria vizuri kuhusu mpango wa uzazi."

    Idadi ya watu walio na uwezo wa kufanya kazi inaendelea kupungua, kuna wazee wengi ikilinganishwa na watoto wanaozaliwa na umoja wa mataifa unasema China itapoteza wafanyikazi wake milioni 63 ifikapo mwaka 2030.

    Idadi ya raia wa wazee wa China pia inatarajiwa kufikia milioni 210 mwaka huo wa 2030 huku mwaka wa 2050 robo ya watu wote nchini humo wakiwa ni wazee.

    Lakini wakati huu serikali inapotoa ruhusa ya kupata watoto wawili ili kuepusha hali ya ukosefu wa nguvu kazi, baadhi ya familia zinaona kwamba malezi ni mzigo mkubwa.

    Bibi Yuan mwenye umri wa miaka 40. Alisema: "Kama hali ya kiuchumi inaruhusu, unaweza kupata mtoto mwingine. Lakini kwa baadhi ya familia, uwezo wao hawawezi kumudu kumtunza mtoto mwingine. Kama mimi, nina mtoto mmoja tu, kutokana na hali yangu ya uchumi, sitaki kuzaa mwingine."

    Serikali bado haijatangaza muda maalum kwa sheria hiyo kuanza lakini utekelezaji wake utakuwa wa taratibu. Hivi sasa hapa China, mmoja kati ya raia kumi ni mzee mwenye miaka 65 na zaidi. Na idadi hii huenda ikaongezeka kwa theluthi moja hadi kufikia mwaka 2050. Wakati huohuo wafanyakazi nao pia wanaendelea kuzeeka.

    Wang Jun, profesa katika chuo kikuu cha Sun Yat-Sen anasema hali hii inasababisha tishio kwa nguvu ya uchumi wa China.

    "Wafanyakazi vibarua na wengine nao pia wanazeeka, jambo ambalo linaweza kuathiri nguvu ya uchumi wa China. Hali hii inaweza kuboreshwa kwa kiasi Fulani kwa kubadilisha sera ya uzazi"

    Mwaka 2013 China ilifanya mabadiliko ya sera kwa kuruhusu watu kuzaa mtoto wa pili hususan wale ambao ni watoto wa pekee kwenye familia zao. Mwanzoni makadirio yalionesha kuwa kwa mwaka watazaliwa watoto milioni mbili baada ya mabadiliko hayo. Lakini ongezeko halisi kwa mwaka jana lilikuwa ni nusu milioni tu. Baada ya wazazi wengi kusema hawawezi kumudu kuzaa mtoto wa pili.

    "Hivi sasa mimi nafanya kazi na mke wangu anamtunza mtoto wetu. kama tukizaa mtoto wa pili, sote wawili itatubidi tufanye kazi na kuajiri mlezi, lakini hatuwezi kumudu jambo hilo."

    Hata hivyo hii haimaanishi kuwa wazazi wengi wako kinyume na sera ya mtoto mmoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako