• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Changamoto anazokabiliana nazo mtoto mlemavu asiye na mikono Elisha Angombi

    (GMT+08:00) 2016-01-12 08:44:44

    Karibu msikilizaji kwenye kipindi hiki cha sauti ya wanawake, hiki ni kipindi kinachokuletea masuala mbalimbali yanayomhusu mwanamke pamoja na mtoto. Na katika kipindi cha leo tutazumngumzia mtoto mlemavu aitwaye Elisha Angombi wa nchini DRC na jinsi anavyokabilia na changamoto mbalimbali katika maisha yake ya kila siku. Zakia ana ripoti zaidi.

    Kwa mujibu wa Shirika la kuwahudmia Watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF, asilimia kati ya 5 na 10 ya watoto wanakuwa wakiwa na ulemavu. Sababu kuu inaaminika kuwa ni pamoja na matatizo ya kimaumbile, matatizo wakati wa kujifungua, magonjwa kama surua na homa ya uti wa mgongo, huduma duni za afya wakati wa ujauzito na baada ya kujifungua lishe duni inayopelekea kudumaa kwa mtoto.

    Mara nyingi watoto wenye ulemavu mafanikio yao ya kusoma ni mabaya yakilinganishwa na watoto wengine kwa sababu shule hazijawekwa kwaajili ya kuwhudumia watoto hao na walimu mara nyingi wanakuwa hawajapewa mafunzo ya kuwashughulikia watoto wenye ulemavu. Mtoto ELISHA ANGOMBI naye ni mingoni mwa watoto hao wenye ulemavu ambaye hana mikono na yupo nchini DRC. Elisha anasoma shule iliyopo jijini Beni. Na bahati nzuri mwandishi wetu Mseke Dide alibahatika kukutana na mtoto huyo pamoja na walimu wake na kuwa na maeongezi nao ya kina.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako