• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchapishaji wa 3D wasaidia watoto walemavu

    (GMT+08:00) 2016-01-26 07:40:31

    Bw. Chen amefanya kazi za uchapishaji wa 3D kwa zaidi ya miaka mitatu, yeye anaendesha kampuni moja ya uchapishaji wa 3D mjini Cangzhou mkoani Hebei. Baada ya kufahamishwa kuwa mtoto mmoja aliyeko mjini Shizuishan mkoani Ningxia, zaidi ya kilomita moja kutoka mji anaoishi yeye anahitaji mkono mmoja wa kuchapishwa, alipokea kazi hiyo, kwani anaona furaha kubwa kuweza kufanya shughuli za utunzaji jamii kwa kutumia uwezo wake. Lakini kumtengenezea mkono wa bandia kwa mtoto aliyeko mbali sana siyo kazi rahisi, na vilevile hali ya ulemavu ya mtoto huyo ni maalum.

    "Mtoto huyo tunamwita 'malaika No. 1', tuliandaa mpango kwa ajili yake, kwani hali yake ni maalum. Ingawa uchapishaji wa 3D ni kama utengenezaji vitu kwa kufuata matakwa tofauti ya watu tofauti, lakini mahitaji ya mtoto huyo yanatakiwa kufanyiwa marekebisho zaidi juu ya msingi wa utengenezaji wake."

    Uwezo mkubwa unahitajika katika kutengeneza mkono wa bandia, Li Lingfeng, rafiki wa Bw. Chen alishiriki kwenye kazi hiyo, hii ikaongeza ushindi wa kutengeneza "mkono huo wa upendo". Li ni mtengenezaji wa mikono bandia, kazi yake kubwa ni kutengeneza na kuunganisha mikono bandia, haswa kwa watu walemavu.

    "Mfupa wake wa metacarpal sio wa kawaida, na kidole chake gumba vilevile sio cha kawaida, hivyo nguvu ya utendaji wa kidole chake itapungua, na kuwa dhaifu. Kalibu ya mkono bandia iliyopo sasa iliyochapishwa kwa njia ya 3D hailingani hivyo tunatakiwa kuirekebisha kalibu hiyo, hili ni jambo gumu."

    Wakifuata picha iliyotolewa na baba wa "malaika No. 1", Bw. Chen na Li walitengeneza sampuli moja, ingawa mtoto huyo anaipenda sana, lakini haikufanya kazi vizuri. Kukabilikana na hali hiyo maalum, Bw. Chen alimwendea rafiki yake ambaye ni daktari wa mifupa, na kumtaka ushauri.

    "Mkurugenzi Wang, hujambo! Huyu ni mwenzangu Li Lingfeng. Hii ni kalibu ya mkono, tafadhali iangalie kama inahitaji kurekebishwa, ama ina upungufu wowote."

    Baada ya kujaribu na kurekebisha mara kwa mara, mkono wa pili wa mashine ulichapishwa, ambao unanyumbulika kuliko ule wa kwanza, mbali na hayo vidole vya mkono huo vumetengenezwa kuwa rangi nyeupe kwa kufuata matakwa ya "malaika No.1".

    "Uchapishaji wa 3D mchakato wake wsio mgumu kiufundi, bali ni ugumu upo katika ubunifu na matumizi. Lakini kutokana na maendeleo ya teknolojia ya sasa, tunaweza kutatua ugumu huo kwa njia ya masafa marefu. Hili ni jambo linalorahisisha maisha yetu, na vilevile ni kitu kizuri."

    Ingawa mkono huo unaonekana kama kidude, lakini una maana kubwa katika shughuli za utengenezaji mikono bandia.

    "Kutokana na uzoefu wangu wa kazi wa miaka mingi, bei za mkono bandia ya zamani ziko juu, na mahitaji ya matumizi ya mikono hiyo ni makubwa mno, lakini uchapishaji wa 3D huenda ukabadilika katika pande hizo mbili. Watoto wataweza kutumia mikono hiyo ya bei rahisi inayoweza kutumika kwa urahisi."

    Bibi Duan Li ni kiongozi wa idara ya matangazo katika kampuni moja inayotoa habari kuhusu uchapishaji wa 3D----3D Tiger. Bibi Duan alimuelezea Bw. Chen hali ya "malaika No. 1" .

    "Mwanzoni tulipopokea nyaraka za mtoto huyu, tulidhani hatutaweza kuchapisha mkono anaouhitaji. Kwa sababu mkono wake huu una kidole kimoja tu, wala hatukujua kama ni kidole gumba ama kidole cha shahada, hii ilihusiana na suala la kuirekebishia kalibu yetu. Tuliwasiliana na viwanda vingi, ambavyo vingi vyao havina madaktari wanaoweza kutoa muongozo. Halafu tulisambaza habari hii kupitia Wichat na PC yetu, mwalimu Chen kutoka mkoa wa Hebei akafahamu hali hiyo, akasema anaye daktari, na wanapenda kumsaidia mtoto huyo."

    "Mwanzaoni tulimwelezea habari hii baba wa mtoto, na kila siku mtoto wake alimuliza baba yake 'mkono wangu utafika lini?'Wakati alipouvaa mkono wake bandia hakutaka kuuvua. Baba yake alimpiga picha, mtoto alikuwa na furaha kubwa, na hakutaka kuuvua, hata wakati anapolala."

    "Hujambo, jitambulie kidogo. Hujambo. Nimepigwa sana, umenipigia umbali."

    "Baada ya kuwa na mkono huo wa mashine, alifurahi sana alipouvaa, akasema 'Baba angalia, nina vidole vinne." Ana furaha mno, hataki kuuvua, kila siku anauvaa hata anapolala. Kwa hiyo nawashuruku sana marafiki waliojitolea kwa ajili ya jambo hili, nakushukuruni."

    "Mama angalia! Mama angalia! Nimeshika dubu kwa mkono."

    "Kwa kupitia mkono huu wa kuchapishwa kwa njia ya 3D, mimi mwenyewe nimekuwa na imani kubwa. Kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia katika siku za mbele, huenda tatizo la mkono wa mtoto wangu halitakuwa tena tatizo."

    "Ingawa hatujaonana, tulikuwa tunakuita 'malaika No.1', tunatumai maisha yako yatakuwa na heri njema zaidi."

    "Natumai utakuwa na furaha na afya njema, na nitaweza kukutengenezea mkono bandia ulio bora zaidi."

    "Natumai utatengeneza miujiza mingi zaidi kwa kutumia mkono wako huu."

    "Nataka kuunga mkono familia zinazofanana nasi, usiogope, wala kuhuzunika, pokea hali ilivyo kwa ushujaa. Kadiri watoto wanavyokua siku hadi siku, utahisi furaha kutoka kwao, utawaona watoto hao hawana tofauti na watoto wengine."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako