• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Eneo la biashara kupitia mtandao wa internet la kijiji cha Qingyuan lasaidia kuanzisha shughuli kwenye mtandao wa internet

    (GMT+08:00) 2016-01-14 10:20:20


    Sehemu ya Qingxin ya mji wa Qingyuan, kaskazini mwa mkoa wa Guangdong China ni sehemu inayozalisha mazao ya kilimo kwa wingi. Sehemu hiyo imezungukwa na milima, na wakazi wa eneo hilo wanajihusisha na kilimo cha matunda na mboga. Watu wanaoishi huko na waliowahi kutembelea eneo hilo wote wanasifu kuwa, hali ya hewa ya huko ni nzuri sana. Madransi na pitaya yenye nyama nyekundu ni matunda bora yanayozalishwa huko, na kilimo cha matunda hayo ni shughuli ambayo wakazi wa huko wanaitegemea.

    Hata hivyo, ingawa sehemu ya Qingxin ina hali nzuri ya kilimo, lakini iko katika eneo mbali la milimani lenye hali ngumu ya mawasiliano ya barabara. Namna ya kuyafanya mazao ya kilimo ambayo wakulima wanayotegemea kwa maisha yao, kufika kwa wateja, kufika sehemu ya kaskazini kutoka sehemu ya kusini, na namna ya kuunganisha bidhaa na masoko vimekuwa suala gumu kwa watu wa Qingyuan.

    Wakati huohuo, meneja mkuu wa Kampuni ya maendeleo ya kilimo ya kiikolojia ya Qiannong Bw. Zhou Zihua alirudi maskani yake kutoka mji wa Hangzhou akiwa na kundi lake la kuanzisha shughuli za kilimo. Safari hii aliamua kushirikiana na wakulima, na kuuza matunda ya Pitaya yenye nyama nyekundu katika masoko yote nchini China. Bw. Zhou anasema,

    "Sisi watu wa Qingyuan hatukosi bidhaa nzuri, ila tu tunakosa namna ya kuzifikisha sokoni. Hetka zaidi ya 200 za matunda ya Pitaya yenye nyama nyekundu za tarafa ya Taiping zinahusu wakulima kati ya 30 na 40. Baadhi yao hata wana hekta zaidi ya 6.67, na wanaopanda kwa uchache wanapanda hekta 0.53 hadi 0.67. Na tunaweza kuuza matunda yetu kilo elfu 25 hadi 30 katika mwezi mmoja. Ikiwa katika kipindi cha mavuno, hata tunaweza kuuza kilo elfu 40 hivi za matunda hayo."

    Uamuzi wa Bw. Zhou Zihua kurudi maskani na kujihusisha shughuli zake, si kama tu kulitokana na hamasa, bali pia alizingatia mazingira yanayoruhusu ujasiriamali katika maskani yake. Mwezi Aprili mwaka jana, eneo la biashara kupitia mtandao wa internet la kijiji cha Qingyuan lilianzishwa rasmi. Eneo hilo limepangwa ili liweze kupokea na kusaidia makampuni 100 kwa wakati mmoja, eneo lake ni mita za mraba elfu 18. Hii ni fursa nzuri sana kwa wajasiriamali wanaorudi maskani kwao. Naibu meneja mkuu wa eneo hilo la biashara Bw. Cheng Chaobing alipozungumzia eneo hilo amesema, eneo hilo limeanzishwa kwa ajili ya kutoa jukwaa la huduma kwa kuunganisha maliasili ya kijiji na makundi ya biashara, ili kutoa huduma za pande zote kwa viwanda vinavyoanzisha shughuli zao. Bw. Cheng anasema,

    "Katika kipindi cha mwanzoni, kazi ya eneo la biashara ni kukusanya viwanda vya kibiashara, na katika kipindi cha baadaye, kazi yake ni kusaidia viwanda hivyo kujiendeleza, kununuliana hisa za viwanda vingine na kulea viwanda, ili viwanda hivyo vikuzwe siku hadi siku. Pia tunatoa jukwaa letu la biashara kupitia mtandao wa internet, linaloitwa 'utafutaji wa maskani', ambalo linashughulikia zaidi uunganishaji wa maliasili ya kijiji na makundi ya wajasiriamali wa mijini."

    Eneo la biashara kupitia mtandao wa internet la kijiji cha Qingyuan linatoa huduma tofauti kwa kufuata mahitaji tofauti ya viwanda vinavyoingia katika eneo hilo katika vipindi tofauti. Kwa mfano, katika kipindi cha mwanzoni wakati kampuni inaanzishwa, eneo hilo linaruhusu kampuni kufanya shughuli zao na kuuza bidhaa zao kwenye jukwaa bila malipo; katika kipindi cha katikati na cha mwisho, ambapo kampuni hiyo inapohitaji kuimarisha ujenzi wa makundi, eneo hilo litatoa mafunzo ili kujulisha kampuni hiyo namna ya kuunda makundi yenye nguvu; katika kipindi cha mwisho, eneo hilo pia linatoa uungaji mkono wa ukusanyaji mitaji kwa kampuni, ili kusaidia kampuni kupata njia endelevu ya kujiendeleza.

    Akiwa mmoja wa wajasiriamali wa mwanzo kuingia katika eneo la biashara kupitia mtandao wa internet la kijiji cha Qingyuan, Bw. Zhou Zihua amesema, njia mbalimbali za kupata habari na mazingira mazuri ya ujasiriamali ni vitu vinavyomvutia. Anasema,

    "Hapa habari ni wazi, na mazingira ya ujasiriamali ni mazuri. Wanasamehe kodi zetu za miaka mitatu. Cha muhimu zaidi ni kwamba linatoa huduma ya kutufahamisha kuhusu wakulima, na kutusaidia kuwasiliana nao. Kwa kufanya hivyo, suala la kutokuwa na taarifa za kutosha litatatuliwa."

    Kwa serikali ya huko, kuanzisha mfumo wa biashara wa pande mbili wa "bidhaa za viwanda zifike vijijini na mazao ya kilimo kufika mijini", kuboresha maisha ya wakulima, na kuinua kiwango cha utoaji huduma ili kiwe sawa kati ya miji na vijiji ni lengo lake la mwisho. Eneo la biashara kupitia mtandao wa internet la kijiji "linaloongozwa na viwanda na kuelekezwa na serikali" ni njia nzuri ya kutimiza lengo hilo. Ili kuhimiza maendeleo ya eneo hilo, serikali imetoa sera nyingi nafuu. Naibu katibu wa kamati ya chama ya wilaya ya Qingxin Bw. Zhang Renjian anasema,

    "Ya kwanza tunatoa ruzuku ya kodi za nyumba, ikiwemo ruzuku ya kodi za nyumba na maghala. Ya pili tunatoa ruzuku ya huduma za umma kwa viwanda, kwa mfano huduma ya internet ndani ya eneo hilo ni bure, na wanafunzi wa vyuo vikuu wakianzisha shughuli zao wanapewa mikopo. Aidha, tunatoa baadhi ya uungaji mkono wa fedha kwa wenye viwanda wanaoanzisha shughuli zao. Kwa mfano wanaanzisha shughuli zao kupitia mtandao wa internet na kuchagua mikopo, tunatoa punguzo kwa riba ya mkopo wao. Wakati huohuo, serikali yetu pia inatoa dhamana ili kuwasaidia vijana kutafuta uungaji mkono kifedha. Kwa ujumla, kila mwaka uungaji mkono wa serikali yetu katika mambo ya fedha kwa eneo hilo unazidi Yuan milioni 4, na kukaribia milioni 5, na tutaendelea kuwaunga mkono kwa miaka mitatu mfululizo."

    Matunda ya Pitaya yenye nyama nyekundu katika kiunga cha miti ya matunda yamekomaa, na yanakaribia kuuzwa kwa wateja wa mijini. Sasa kuna jukwaa la biashara kupitia mtandao wa internet, na limeunganishwa na masoko, lakini Bw. Zhou Zihua ana mawazo mengine. Anatumai kuwa serikali, eneo la biashara na viwanda vinavyoingia katika eneo hilo vinaweza kutoa fedha kwa pamoja kwa ajili ya kujenga kituo cha usambazaji bidhaa, kwa kufanya hivyo, wafanyabiashara wote wa mazao ya kilimo wa huko watapata faida, na wanaorudi makwao kujihusisha na ujasiriamali pia wana nguvu zaidi ya ushindani katika masoko.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako