• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kijiji kizuri cha Wentong mjini Wanning mkoani Hainan

    (GMT+08:00) 2016-01-28 10:44:40

    Tukizungumzia mambo ya kijiji, huenda bado unayofikiria ni picha ya "takataka kila mahali na kutokuwa na utaratibu". Lakini nchini China kadiri vijiji vinavyoendelezwa, ndivyo mwamko wa wakulima kuhifadhi mazingira wanayoishi na mazingira ya asili inavyoinuka. Hali ya kimaumbile vijijini inazidi kuwa nzuri siku hadi siku, na kiwango cha maisha ya wakulima pia kinainuka siku hadi siku. Katika kisiwa cha Hainan, kuna kijiji kimoja kizuri, ambacho kinatoa bure huduma ya WIFI, pia kuna picha za QR code zilizobandikwa mbele ya mimia ya aina mbalimbali ambazo watalii wanaweza kutambua mimea hiyo kwa kuzipigia picha kwa kutumia simu ya mkononi.

    Kijiji hicho kinaitwa Wentong, kiko kusini magharibi mwa tarafa ya Changfeng mjini Wanning mkoani Hainan, umbali wa kilomita 2 kutoka sehemu ya vivutio ya Xinglong. Hicho ni kijiji chenye mandhari nzuri cha kabila la Wali. Kijiji hicho kina familia 56 zenye watu 208, kina maliasili nyingi nzuri, lakini kutokana na wakazi wake kuwa na mtazamo wa jadi, shughuli zilizofanyika kwenye kijiji hicho ni chache na zilikuwa nyuma kimaendeleo. Katibu wa kamati ya kijiji hicho Bw Huang Yeping alipozungumzia hali ya kijiji cha Wentong ilivyokuwa kabla ya mwaka 2009, alisema,

    "Kabla ya mwaka 2009, kijiji chetu hakikuwa na barabara, takataka zilizagaa kila mahali, na hakikuwa na utaratibu. Kiwango cha maisha ya wanakijiji wetu kilikuwa cha chini, na wastani ya mapato yao kwa mwaka haukufikia Yuan 2,000. Wengi waliishi kwa kutegemea kilimo."

    Kabla ya mwaka 2009, barabara na miundo mbinu mingine ya umma ilikuwa mibovu, na hali ya usafi kijijini pia ilikuwa mbaya, hayo yote yaliathiri vibaya mazingira ya kijiji. Bw. Huang Yeping alifahamisha kuwa, baada ya mwaka 2009, kijiji cha Wentong kilianza kuboresha uzalishaji, hali ya mazingira ya asili na maisha ya watu wa kijijini, na kuunganisha ujenzi wa ustaarabu wa kiikolojia pamoja na uhimizaji wa maendeleo ya miji na vijiji, ujenzi wa utamaduni wa kijiji, maendeleo endelevu na ongezeko la mapato ya wakulima. Kwa kufuata hali halisi, kijiji hicho kimejenga barabara mpya zenye miti katika kando mbili na kuwa vivutio, na pia kimepanda maua na miti mbalimbali mbele na nyuma ya nyumba, ili kufanya mandhari ya kijiji kuwa nzuri; vilevile kimejenga mfumo wa kushughulikia maji taka na mradi wa ardhi oevu, na kuongoza wanakijiji kubadili njia zao za uzalishaji na maisha. Hivi sasa, ujenzi wa ustaarabu wa kimazingira wa kijiji hicho umepata maendeleo makubwa, na maisha ya kitamaduni ya wanakijiji pia yamekuwa mazuri siku hadi siku.

    Kadiri chumba cha burudani cha kijiji, jumba la maonesho na kiwanja cha mpira wa kikapu na mpira wa wavu vinavyojengwa na kutumiwa, pamoja na kufanyika kwa shughuli za utamaduni vijijini, kusoma vitabu na magazeti, kucheza mpira na chesi, na kucheza ngoma ndivyo kumekuwa njia mpya za maisha ya wanakijiji wakati wanapopumzika, na sura ya kijiji imebadilishwa kuwa nzuri zaidi. Mwanakijiji wa kijiji hicho Wang Xiaoyan alipozungumzia mabadiliko hayo anasema,

    "Tulijenga nyumba yetu mwaka 2012 kutokana na uungaji mkono wa serikali. Kabla ya hapo, kando za nyumba yetu ya zamani kulikuwa na nyasi, na baada ya kutusaidia kujenga nyumba, serikali pia ilijenga barabara. Sasa maji, umeme na barabara vyote vimefikishwa kijijini, na pia tumepanda miti mingi."

    Sehemu ya utalii ya Xinglong inapoendelezwa, inatumia ubora wa kijiografia wa kijiji cha Wentong, na kukiunganisha kijiji hicho katika ujenzi wa utaratibu wa burudani wa Xinglong. Inawasaidia wanakijiji kuendeleza miradi ya utalii na burudani kijijini, na kurekebisha mabwawa ya samaki ya kijijini kuwa kituo cha uvuvi cha maji baridi. Pia imefanikiwa kuingiza Kampuni ya kilimo cha burudani ya Ndoto ya Hainan, kuendeleza na kujenga miradi mbalimbali ya utalii wa kijijini kwa njia ya ushirikiano kati ya kijiji na kampuni. Kupitia utalii wa kijiji, kijiji cha Wentong si kama tu kimesaidia wanakijiji wa kijiji hicho kuongeza mapato yao, bali pia kimesaidia baadhi ya wanakijiji kupata ajira. Mwaka 2014, idadi ya watalii waliotembelea kijiji hicho ilifikia zaidi ya elfu 30, na wastani ya mapato ya wakulima ulikuwa zaidi ya Yuan 8,000.

    Wakati kinapozingatia hali ya viumbe na maendeleo ya uchumi, kijiji cha Wentong pia kinatilia maanani kuhifadhi utamaduni wa jadi, na kuheshimu mila na desturi za wanakijiji. Msaidizi wa katibu wa kamati ya kijiji cha Wentong Wu Haiping anasema,

    "Kijiji hicho kinahifadhi umaalum wetu wa kabila la Wali, maisha, utamaduni na urithi wenye umaalum wa kabila la Wali yote tumehifadhi."

    Ni kuhifadhi kwa nguvu kubwa hali ya viumbe na utamaduni wa jadi, ndiyo maana mwaka 2014 kijiji cha Wentong kilichukuliwa kama "kijiji chenye umaalum wa makabila madogomadogo ya China", na kutajwa kuwa moja ya "vijiji kumi bora nchini China". Hivi sasa kijiji cha Wentong kimepata sifa nyingi kama vile "kijiji cha kiikolojia", "kijiji cha jadi" na "kijiji chenye mandhari nzuri". Mwandishi wetu wa habari alipoingia katika kijiji hicho, aligundua kuwa kijiji hicho hata kina huduma ya WIFI bure, na mbele ya baadhi ya mimea kuna picha za QR code kwa watalii ku-scan. Bibi Wu Haiping alifahamisha kwa fahari akisema,

    "Sasa kote kijijini kuna huduma ya WIFI, na WIFI hiyo inatolewa na idara husika na idara ya mawasiliano ya habari kwa wanakijiji wetu, vilevile kwa kuwa sisi hapa ni sehemu ya kitalii ya kijiji, hivyo zinatupatia WIFI. picha za QR code za mimea, yaani watalii waki-scan picha hizo, wanaweza kujua habari husika za ukuaji, jina la kiingereza, na kipindi cha kuchanua na kukomaa cha mimea, na QR code hizo zinaunganishwa kwenye mtandao wa mbuga ya mimea ya tropiki ya Xinglong."

    Ili kuwarahisishia wanakijiji na watalii, kijiji cha Wentong kinakwenda na wakati na kutumia teknolojia ya mtandao wa internet ili kujiimarisha. "Kijiji kipo misituni, nyumba zimezingirwa na miti na watu kama wanaishi katika michoro" ndiyo picha halisi ya kijiji cha Wentong cha hivi leo. Inaonesha wazi kuwepo kwa pamoja kwa mila za jadi na mambo ya kisasa, na uwiano kati ya hali ya viumbe na maendeleo. Mwisho wa kipindi chetu, msaidizi wa katibu wa kamati ya kijiji cha Wentong Wu Haiping anatoa mwaliko kwa watalii wote duniani akisema,

    "Nawakaribisha, marafiki wote duniani, nawakaribisha mtalii katika kijiji chetu cha Wentong kutalii. Tuna WIFI, picha za QR code za mimea mbalimbali, pia tuna kahawa na chai maalum ya Partridge, kwa niaba ya wanakijiji wenzangu nawakaribisha marafiki wote duniani."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako