• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soko la China: fursa kwa wazalishaji wa Afrika inayohitaji kufanyiwa kazi zaidi

    (GMT+08:00) 2016-01-29 20:09:40
    Mwezi Desemba mwaka jana mkutano wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika ulifanyika mjini Johannesburg nchini Afrika Kusini. Moja kati ya mambo yaliyojadiliwa ni kuhakikisha kuwa thamani ya biashara kati ya pande hizo mbili iongezeke kutoka dola za kimarekani bilioni 220 za mwaka 2014, hadi kufikia dola za kimarekani bilioni 400 ifikapo mwaka 2020. 

    Licha ya kuwa thamani ya biashara kati ya China na Afrika ni kubwa, kiwango cha biashara kati ya pande hizo mbili kinaweza kuendelea kuongezeka. Pande mbili zilijadili hatua zinazoweza kuchukuliwa ili kuhimiza biashara. Moja ya hatua hizo ni kuimarisha huduma za usafiri kati ya pande mbili. Ingawa watu wanaosafiri kati ya China na Afrika wanazidi kuongezeka, usafiri wa moja kwa moja kati ya pande hizi mbili si wa kuridhisha. Wasafiri wengi wanalazimika kupitia Ulaya au mashariki ya kati. Tatizo hilo linaendelea kupunguzwa kwani, kwani baadhi ya mashirika ya ndege ya nchi za Afrika, Shirika la ndege la Kenya na shirika la ndege la Ethiopia yanafanya safari za moja kwa moja kati ya nchi hizo na China. Lakini mashirika ya ndege ya China yanafanya juhudi kuongeza safari za kwenda Afrika. Mbali na ndege za Shirika la ndege la China linalofanya safari za moja kwa moja kati ya China na Afrika kusini na Ethiopia, mwaka jana shirika la ndege la China Kusini lilianzisha safari kati ya mji wa Guangzhou na Nairobi.

    Licha ya China kutangaza orodha ndefu ya bidhaa zinazoweza kuingia kwenye soko la China bila ushuru, bado kuna changamoto ya utaratibu wa forodha kwa bidhaa za Afrika kuingia kwenye soko la China. Kwa sasa pande mbili zimekubaliana kuhimiza hatua ukaguzi wa bidhaa na karantini ili kuhimza bidhaa za chakula na kilimo kuweza kuingia kwa urahisi. China pia inafanya juhudi ya kuanzisha miradi 50 ya kuhimza biashara katika sehemu mbalimbali za Afrika. Miradi hiyo mbali na kuvutia uwekezaji na teknolojia kutoka China, pia vinatarajiwa kuhimiza uzalishaji na usafirishaji wa bidhaa za Afrika kuingia kwenye soko la China.

    Tukiangalia hali ya jumla ya China inavyojipanga katika kushirikiana na nchi za Afrika, unaona kabisa kuwa serikali ya China haijiweki pembeni kuwasaidia wafanyabiashara wanaotaka kuwekeza na kufanya biashara Afrika. Kwa mfano kuna Mfuko wa Maendeleo kati ya China na Afrika CAD Fund, mfuko huu unalenga kuwasaidia wafanyabiashara wa China wanaotaka kuwekeza kwenye miradi ya maendeleo katika nchi za Afrika, hasa miradi inayozinufaisha pande zote mbili. Mfuko huu unataja wazi ni maeneo gani ambayo yanapewa kipaumbele, na hata namna ya kuwasaidia wachina wanaotaka kufanya biashara katika nchi za Afrika.

    Lakini tukiangalia upande wa nchi za Afrika, ni vigumu kuona mpango uliowazi wa kutumia na kunufaika na soko la China. Bado nchi za Afrika hazina mfuko unaofanana na CAD fund, japo kusaidia wafanyabiashara wenyewe kuuza bidhaa zao China, au hata utaratibu unaotaja ni bidhaa gani ambazo inaweza kutoa msukumo na kuhimiza uzalishaji wake, kuwahamasisha na kuwasaidia watu kuzalisha bidhaa hizo ili tutumie soko la China. Serikali inaweka mkazo kwenye sera za jumla (macro policies), lakini kuwa na sera peke yake bila hatua za kuisukuma sera hiyo, hatuwezi kuwa na matokeo yoyote ya maana. Wakulima na wafanyabiashara hawafahamishwi wazi kuhusu fursa zilizopo, na wachache wanaofahamu hawasaidiwi kunufaika na fursa hizo. Matokeo yake ni kuwa fursa ipo, na haitumiwi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako