• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika asema haki ya wanawake ni muhimu kwa maendeleo ya Afrika

    (GMT+08:00) 2016-02-02 07:34:59

    Mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Bibi Dlamini Zuma amewataka viongozi wa nchi za Afrika kuhakikisha haki za wanawake zinaheshimu katika nchi zao. Bi Zuma amemtaja mwanamke kuwa nguzo muhimu katika maendeleo ya jamii na kusisitiza haja ya kuhakikisha anachukua nafasi yake katika ajenda ya maendeleo ya mwaka wa 2063. Kwa maelezo zaidi kuhusu habari hiyo huyu hapa Jacob Mogoa akiripoti kutoa Addis Ababa, Ethiopia.

    Bi Zuma amesisitiza kuwa ajenda ya 2063 ni ya wanawake wakiwemo kina mama na wasichana ambao wamekuwa wakionyesha uvumilivu maishani na kuwajali wengine katika jamii. Anasema sifa hiyo imewafanya kustahimili hali ngumu za maisha na kukabiliana na changamoto nyingi maishani. Sifa hiyo, Bi Zuma anasema imekuwa na mchango mkubwa katika jamii.Anasema bila mwanamke ni vigumu kufikia mabadiliko tuyatakayo.

    "Ajenda ya 2063 ni ya wanawake na wasichana wenye ujasiri na wanaotilia maanani mabadiliko. Pia ni ya wale wenye nia ya kutafutia watoto wao maisha mema, kufaidi jamii zao na kutupa changamoto sisi wote. Bila wao kuwajibika na kujumuika kwenye ajenda hii, mabadiliko yetu yatakuwa ya chini sana na yasiyo na faida kwa binadamu.Vuguvugu la wanawake na jinsia limekamilisha vikao vyake hivi majuzi. Suala lililoangaziwa sana ni maendeleo ya mwaka wa 2015 haswa uwezeshaji wa wanawake wa bara hili. Mataifa yetu yanaangazia sana haki za wanawake, kama vile kumiliki mashamba, usawa wa mishahara kazini, kufanya biashara, teknolojia ya kilimo na kupata elimu bora . Tuataendelea kupigania haki hizi na kuhakikisha vifo vya kina mama wajawazito vinatokomea.Pia tunaangazia masuala kama maji safi ya kunywa, mazingira na kawi inayoeza kufikika. Tunaamini haya ni muhimu kwa jamii".

    Kwa mujibu wa Umoja wa mataifa, wanawake wengi wamekuwa wakiteseka katika nchi zinazokumbwa na migogoro kama vile Sudan Kusini, Burundi na Jamhuru ya kidemokrasia ya Kong DRC.Ombi hilo la Bi Zuma pia linakuja muda mfupi tu baada ya serikali ya DRC kuchukua hatua za kisheria dhidi ya watu wanaotuhumiwa kuwabaka wasichana wadogo mkoani Kivu kusini. Aisha Laraba Abdulahi ni kamishna wa masuala ya Siasa wa Umoja wa Mataifa. Anasema Umoja wa Afrika umejadili kwa upana jinsi ya kuhakikisha haki za mwanamke zinalindwa ipasavyo.

    "Tuna mambo mengi yenye uzito kwetu sisi. Mambo ambayo wengine wanaona yana uzito kwao kwetu huenda yasiwe na uzito.Maswala yanayohusiana na tadamaduni zetu,kuoza wasichana wadogo mapema ni baadhi tu ya masuala tunayopaswa kushughulikia. Suala la ukeketaji linapaswa kukabiliwa na kukemewa. Maswala mengine ni yale yanayohuasiana na haki ya kupata chakula, kuwa na makazi, kupata elimu bora na haki ya kuwa na nishati.Kina mama wanaotoka mataifa wanachama wanalazimika kutembea mwendo mrefu sana kutafuta kuni ili kupikia familia zao. Kwa hiyo ustawishaji wa kawi ni jambo muhimu sana. haya ndio mambo tunayopaswa kushughulikia kwanza".

    Kutokana na vikwazo vya kijamii, kiuchumi, kimazingira, kijiografia na kimila, wasichana wa kiafrika wanaendelea kukumbwa na hali ya juu ya ukosefu wa ajira au ajira duni, pamoja na ukosefu wa huduma za elimu bora, mtaji, na huduma za afya ikiwemo afya ya uzazi.Hata hivyo katika baadhi ya nchi wanawake wamejitahidi kupigania haki zao na hatimaye kufanikiwa kuchukua uongozi katika sekta za uchumi, siasa, au ustawi wa jamii. Bi Zuma anapongeza nchi za Ethiopia na Sudan Kusini kwa kuonyesha mfano mwema katika kumshirikisha mwanamke katika masuala ya maendeleo na uongozi wa nchi zao. Anasema hii ndio njia pekee ya kuhakikisha Afrika kwa pamoja inapiga hatua za kufikia maendeleo yanayoonekana.

    "Tangu tulipoanzisha mkutano wa kwanza wa kutathmini masuala ya kijinsia mwaka jana nchi nyingi zimechukua hatua ya kurekebisha hali katika nchi zao. Kati ya chaguzi kumi zilizofanyika mwaka jana Afrika ni Ethiopia na Sudan Kusini pekee ambazo zimeongeza idadi ya wanawake bungeni. Hatua hiyo imezifanya nchi hizo kuingia katika kundi la nchi zenye zaidi asilimia 10 ya wanawake bungeni. Tunafaa kuweka juhudi zaidi katika mwaka huu wa 2016".

    Miaka 20 baada ya mkutano wa Beijing, Umoja wa mataifa unasema hakuna nchi hata moja duniani ambayo imefikia usawa wa kijinsia. Hata hivyo wachambuzi wa masuala ya kijinsia barani Afrika wanasema mafanikio kadhaa yameshuhudiwa hususan upande wa elimu ya wasichana, vifo vya wanawake wajawazito au ukatili wa kijinsia, lakini tofauti za kijinsia bado zinakumba maisha ya wanawake wengi duniani hasa katika nchi zinazoendelea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako