• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kijana wa Iran aliyeanzisha familia yake mjini Beijing

    (GMT+08:00) 2016-02-02 19:55:47

    China na Iran ni nchi zenye ustaarabu wa siku nyingi, na zimejenga urafiki mkubwa kupitia mawasiliano kwenye njia ya hariri ya kale. Kutokana na kuimarishwa kwa maingiliano kati ya nchi hizo mbili, katika miaka ya hivi karibuni, watu wengi zaidi kutoka Iran wamekuja China kufanya kazi au kuendelea na masomo, na kijana Abuo Bakr Ravand ni mmoja kati yao. Wakati akiwa masomoni hapa Beijing, Bw. Ravand si kama tu amependa maisha ya Beijing, na pia amepata mpenzi wake na kuanzisha familia yake hapa nchini China.

    Bw. Bakr Ravand aliwahi kuwa mwanariadha wa timu ya taifa ya Iran, na aliiwakilishi Iran mara nyingi kushiriki kwenye mashindano ya kimataifa. Baada ya kustaafa mwaka 2010, alikuja China kusoma shahada ya udaktari kuhusu mafunzo ya michezo kwenye chuo kikuu cha michezo cha Beijing. Mpaka sasa ameishi mjini Beijing kwa miaka zaidi ya 5, Bw. Ravand anaona kuwa Beijing ni mji wa kupendekeza wenye mambo mengi ya kale.

    "Beijing ni mji mzuri sana, hapa kuna mambo mengi ya kale. Napapenda sana Beijing, haswa uwanja wa michezo wa Bird's nest, bustani ya misitu ya Olimpiki, Ukuta mkuu, mtaa wa Sanlitun, Kasri la kifalme The Forbidden City na kadhalika."

    Akiwa mwanariadha mstaafu wa mbio ndefu wa timu ya taifa ya Iran, kukimbia kweli kumekuwa tabia ya maisha ya Bw. Ravand. Anaona kwamba kukimbia kunaweza kuwafanya watu wawe karibu na maumbile, na kubadili maisha yao.

    "Kukimbia ni mchezo huru, hauna vizuizi vyovyote. Inachohitaji ni viatu vya kukimbia tu. Unaweza kukimbia milimani, unaweza kukimbia ufukweni, pia unaweza kukimbia mitaani, unaweza kwenda mahali popote unapotaka. Wakati wa kukimbia, utasahau usumbufu wowote, na kujitumbuiza kabisa na furaha ya mchezo huo. Kwangu mimi, kukimbia ni kila kitu, na maisha yangu yamebadili kutokana na mchezo huo. Mafanikio yangu yote pia yamepatikana kwa kukimbia."

    Kuna msemo wa kichina usemao "watu wenye hatma ya kuoana hukutana licha ya umbali unaowatenganisha". Kwa Bw. Ravand kutoka Iran, msemo huo unafaa kabisa kuelezea jinsi alivyopata mpenzi wake mchina, na tabia ya pamoja ya kufanya mazoezi ya kukimbia ndiyo inayowakutanisha. Bw. Ravand amesema, kabla ya kuja China, aliwahi kufikiria kwamba huenda atakutana, kupendana na kuoa msichana kutoka China.

    "Tulianza kupendana wakati tulipokuwa tukisoma katika chuo cha michezo cha Beijing, wakati huo alikuwa anafanya mazoezi na kukimbia mara kwa mara kwenye uwanja, kadri ziku zilivyoenda tulifahamiana, mimi pia napenda kukimbia, kwa hiyo nilikuwa nakimbia mara kwa mara kwenye uwanja ili kuweza kukutana naye."

    Wakati Bw. Ravand alipokuwa akimfuatilia kisirisiri msichana anayependa, msichana huyo aitwaye Liu Shuo kutoka mkoa wa Heilongjiang pia alianza kufuatilia Bw. Ravand anayekimbia kama upepo.

    "Kila mara nilipomwona, alikuwa anakimbia kwa majini sana, na pia alipendeza sana. Wakati alipokuwa hakimbii na kuongea nasi, alionekana kuwa ni mkarimu sana. Kope zake ndefu zinapendeza sana, na amenivutia. Napenda kumwangalia akikimbia, naona anapendeza zaidi wakati akikimbia. Yeye ni mwanaume kama upepo. Napenda kuendelea kufuata nyayo zake, na kuwa pamoja naye."

    Katika siku zilizofuata, Bw. Ravand alikuwa anaongea mara kwa mara na msichana huyo mwenye tabasamu kuhusu masomo ya lugha ya kichina, na kadri muda ulivyoenda, watu hao wawili wakapendana. Kwa maoni yao, tofauti za nchi wanazotoka si shida.

    "Binafsi naona kwamba, bila kujali mchumba wangu anatoka nchi gani, muhimu zaidi ni uvumilivu na maelewano. Kwa hiyo naona, sijali kama yeye ni muiran, mchina, mmarekani, au mwafrika, matarajio yetu na hisia zatu za mapenzi ni sawa, kama tukiweza kuelewana na kuaminiana, hili ndilo jambo muhimu kabisa. Ravand amenipa maisha na upendo ninaotaka."

    "Kila mtu ana uelewa wake kuhusu upendo, kwangu mimi, kama unamkumbuka mtu fulani moyoni kila wakati, haswa wakati huwezi kumwona, kutaka kumsaidia wakati anapokumbwa na matatizo, kutaka kumfajiri wakati anapopatwa na huzuni, na kutaka kuwa pamoja naye wakati anapohisi upweke, naona huu ndio upendo. Hizi pia ni hisia zangu kwa mpenzi wangu. Namtaka afurahi kila anapkuwa nami."

    Hivi sasa Bw. Ravand na Bi. Liu Shuo wanafanya kazi hapa Beijing, lakini pia wanaendelea na desturi yao ya kukimbia baada ya kazi.

    "Hivi sasa tunafanya kazi pamoja katika kampuni moja inayotoa mafunzo kuhusu mazoezi ya nguvu ya mwili, mimi ni kocha mkuu. Kazi yetu ni kuweka mpango wa mazoezi ya mwili kwa watoto wenye umri wa miaka 6 hadi 12, kwa kupitia kucheza michezo mbalimbali, tunalenga kuinua ustahimilivu na nguvu ya mwili wao."

    Wakizungumzia maisha ya siku za baadaye, wanandoa hao wana matarajio mengi. Bi. Liu Shuo anatumai kuwa na nyumba yao yenye vyumba vikubwa vinavyotandikiwa zulia la kipersia, na pia wanatarajia kuwa na mtoto wao mwenye kope ndefu kama Ravand. Liu Shuo anasema, mji wa Beijing unawafaa sana, na wataendelea kuishi hapo.

    "Naona Beijing ni mji unaoendelea kwa kasi na wenye fursa nyingi, na mume wangu anaifahamu sana Beijing, kwa hiyo Beijing inatufaa sana, tumechagua kuishi hapa Beijing."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako