• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makampuni ya kichina yaandaa mkakati wa kupanua soko lao nchini Marekani

    (GMT+08:00) 2016-02-03 09:15:04


    Maonesho ya Kimataifa ya Bidhaa za Kieletroniki ya Marekani CES yalifanyika mwezi uliopita mjini Las Vegas, ambapo makampuni kutoka China yalichukua theluthi moja ya washiriki wote wa maonyesho, na yamelichukulia soko la Marekani kama kipaumbele kwenye mikakati yao ya kimataifa.

    Maonesho ya Kimataifa ya Bidhaa za Kieletroniki ya Marekani yamechukuliwa kama mwongozo wa sekta ya bidhaa za kielektroniki, na yamevutia zaidi ushiriki wa makampuni ya China katika miaka ya hivi karibuni. Katika siku ya vyombo vya habari vya maonyesho ya mwaka huu, mikutano iliyoitishwa na makampuni ya kichina kama vile Huawei, ZTE na Letv ilihudhuriwa na waandishi wengi. Aliyekuwa mchezaji wa timu ya Chicago Bulls katika ligi kuu ya mpira wa kikapu ya Marekani NBA Scottie Pippen pia alishiriki katika mkutano wa kampuni ya ZTE. Akizungumzia kampuni hiyo ambayo ni mzalishaji mkubwa wa simu za mkononi nchini Marekani, Pippen anasema,

    "ZTE imefanya vizuri sana, na imepata njia ya kuingia kwenye soko la Marekani na kufanya ushirikiano na timu nyingi za NBA. Katika pande mbalimbali, ZTE ni chapa nzuri."

    Maonyesho hayo sio tu ni fursa nzuri kwa makampuni ya kichina kuongeza ushawishi wao, bali pia ni jukwaa kwa makampuni hayo kuuza bidhaa zao nje ya nchi. Makampuni mengi yalionesha bidhaa zao zilizozalishwa kwa lengo la kupata soko nje ya nchi kwenye maonyesho hayo, kwani soko la Marekani ni muhimu zaidi duniani.

    Kampuni kubwa ya tatu ya simu ya mkononi duniani Huawei ilitoa simu aina ya Mate 8 inayolenga soko la Marekani huku kampuni ya ZTE ikitoa mpango uitwao CSX, ukihamasisha wateja wa Marekani kushiriki katika mchakato mzima kutoka usanifu hadi uuzaji. Kampuni ya uvumbuzi na teknolojia ya Dji kutoka mjini Shenzhen ni mzalishaji mkubwa zaidi wa ndege ndogo isiyo na rubani duniani, na inapanga kushirikiana na kampuni ya magari ya Ford ya Marekani ili kufanya magari na ndege isiyo na rubani viweze kuwasiliana. Kampuni ya Letv iliyoshiriki kwa mara ya kwanza kwenye maonyesho hayo ilionesha runinga nyembamba zaidi duniani, na kutangaza kufanya ushirikiano wa kimkakati na kampuni ya magari ya umeme ya Faraday Future katika siku zijazo.

    Akizungumzia sababu ya kutilia maanani soko la Marekani, naibu mkuu wa kampuni ya Letv Ablikim Ablimit amesema kampuni hiyo inatakiwa kufahamu jinsi wateja wanavyojisikia wakati wa kutumia bidhaa zao.

    "Wakati makampuni mengi ya kichina yanashindwa kuingia kwenye soko la Marekani, kampuni yetu bado inatarajia kuingia katika soko hilo, na kutumia rasilimali na nguvu zote ili kuongeza soko la Marekani, sababu ni kwamba hapa ni eneo lenye mgawanyo wa kazi wenye taaluma ya ngazi ya juu lakini miuundo ya kiviwanda usiobadilika, pia ni eneo ambako uvumbuzi unaweza kufanyiwa kati ya sekta tofauti, hivyo kampuni ya Letv inataka kuja na kujaribu."

    Naibu mkuu wa kampuni ya mawasiliano ya simu ya ZTE Cheng Lixin anasema Marekani ni soko kubwa la wateja, na inaongoza duniani kwa uvumbuzi wa chapa. Amesema mafanikio kwenye soko la Marekani yanaweza kuhimiza mafanikio ya kampuni ya ZTE katika masoko mengine duniani.

    ZTE iliwahi kufanyiwa vitendo visivyo sahihi nchini Marekani ikiwemo kuchunguzwa na bunge, lakini imekua kampuni kubwa ya nne ya simu nchini Marekani baada ya kuendesha shughuli zao miaka kadhaa nchini humo. Bw. Cheng anasema uzoefu wenye mafanikio wa ZTE katika soko la Marekani unaonesha kuwa, kwanza ni lazima kuandaa mkakati unaoendana na hali halisi ya soko linalolengwa, pia kampuni iwe na uwezo wa kufanya uvumbuzi na msingi imara wa hataza. Akizungumzia matarajio ya baadaye ya ZTE katika soko la Marekani, Bw. Cheng anasema kwa imani,

    "Sasa kampuni yetu ya ZTE inashika nafasi ya nne tu, hii haitoshi, na tunatarajia kuwa katika miaka miwili au mitatu ijayo, tutaweza kushika nafasi ya tatu, tuna imani ya kutimiza lengo hilo."

    Hata hivyo, naibu mkurugenzi wa kampuni ya Letv Ablikim Ablimit amekiri kuwa makampuni ya kichina yanakabiliwa na changamoto mbili kuingia katika soko la Marekani. Kwanza ni kuwa makampuni ya China ya kutengeneza vifaa hayana uwezo wa kufanya uvumbuzi na utafiti kama makampuni makubwa ya Marekani ikiwemo Apple, na pili ni kuwa soko la Marekani lina bidhaa za aina mbalimbali, na kama makampuni ya kichina yanataka kupata faida kubwa, hayawezi kushindana na makampuni mengine katika soko hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako