• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mweledi wa tiba ya akupancha ya kichina anayetoka Iran

    (GMT+08:00) 2016-02-04 20:27:12

    China na Iran zote ni nchi zenye historia ndefu, na urafiki kati ya nchi hizo mbili umedumu tangu zamani. Kutokana na kuongezeka kwa mawasiliano kati ya nchi hizo, watu wengi zaidi wa Iran wamekuja China, wakienea miji mbalimbali na kwenye sekta mbalimbali. Tiba ya akupancha ambayo ni moja ya matibabu ya jadi ya kichina, pia imewavutia madaktari wa Iran.

    Dokta. Amirreza Golchian alihitimu chuo kikuu cha udaktari cha Mashhad cha Iran mwaka 1994, katika miaka 10 iliyopita, alikuwa anatoa huduma za matibabu kwenye sehemu za vijijini. Wakati huo aligundua kwamba magonjwa mengi hayatibiki kwa njia ya matibabu ya kimagharibi. Kuanzia hapo, akaanza kutafuta taarifa za matibabu mbalimbali kwenye mtandao wa Internet, na alisoma makala nyingi kuhusu matibabu ya jadi ya kichina. Ingawa wakati huo kulikuwa na tasnifu nyingi za kitaaluma zinazosema kwamba hakuna uthibitisho wa hakika kuhusu ufanisi wa tiba ya akupancha, na hata kulikuwa na habari za kupotosha tiba hiyo. Lakini pia kulikuwa na kesi nyingi za mafanikio ya tiba hiyo ambazo zimetambuliwa kitaaluma. Bw. Amirreza akaanza kuvutiwa na kuwa na hamu ya kujifunza tiba hiyo.

    Mwaka 2005, Dokta. Amirreza alipata fursa ya kujifunza matibabu ya jadi ya kichina hapa Beijing, bila kusita alichagua mara moja tiba ya akupancha. Mwanzoni, Dokta. Amirreza alishuhudia kesi nyingi zenye ufanisi wa kushangaza za aina hiyo ya tiba, na kumfanya aone tiba hiyo ni ya ajabu. Lakini kwa kuwa tiba ya akupancha ina mfumo wa nadharia ulio tofauti kabisa na ule wa matibabu ya kimagharibi, ilimchukua Dokta. Amirreza miaka miwili kuzifahamu na kuzielewa nadharia zake. Baada ya hapo, akaanza kuwa na ufahamu zaidi kuhusu tiba ya akupancha.

    "Kwetu sisi wageni, hatuna fursa nyingi za kuja China kujifunza matibabu ya jadi ya kichina. Nikiwa masomoni hapa Beijing, walimu wengi walinisaidia sana. Mpaka sasa, kila ninapokumbwa na matatizo, ninaomba msaada kutoka kwa mwalimu wangu Bw. Zhao Baixiao, ambaye alinisaidia sana kwenye masomo yangu. Hadi sasa bado naendelea kumtafuta mara kwa mara, na kumwuliza kuhusu matatizo ninayokutana nayo ninapotoa matibabu ya akupancha."

    Akiwa daktari wa matibabu ya kimagharibi, Dokta. Amirreza amefahamu vizuri matibabu ya akupancha, baada ya kurudi Iran, ustadi wake wa kimatibabu umesifiwa sana na wagonjwa aliowatibu. Hali hiyo imemtia moyo sana juu ya matibabu hayo ya kimashariki. Akizungumzia teknolojia mpya ya kutumia tiba ya akupancha kupunguza uzito, Bw. Amirreza amesema,

    "Nilipokuwa nasoma tiba ya akupancha, bado hakukuwa na tiba hii mpya iitwayo Acupoint catgut-embedding therapy. Tiba hiyo ina ufanisi mkubwa hasa kwa kupunguza uzito, katika miaka 10 iliyopita hakukuwa na daktari aliyejaribu kutumia tiba hiyo, lakini sasa madaktari wengi wameanza kuitumia. Kweli ina ufanisi mkubwa wa kusaidia kupunguza uzito."

    Kuanzia mwaka 2012 Dokta. Amirreza alifundisha maneno ya tiba ya kiingereza kwenye kitivo cha mahusiano ya kimataifa cha Chuo kikuu cha matibabu ya jadi ya kichina cha Beijing. Wanafunzi wake wanatoka nchi na sehemu mbalimbali duniani, na karibu wote wamevutiwa sana na tiba ya akupancha. Katika madarasa yake, Dokta. Amirreza pia anafundisha ustadi wa kimsingi wa akupancha.

    "Unaweza kugusa ngozi ya wagonjwa kutafuta acupoint, halafu kama hivi unachoma sindano kwenye acupoint, inauma? Kwa kweli haiumi kabisa, unatakiwa kuchoma sindano kwa kina zaidi kama hivi, sasa niambie kama umehisi kidogo kama umegusa umeme?"

    Hivi leo, Bw. Amirreza ameuchukulia mji wa Beijing kama maskani yake ya pili, na anasafiri mara kwa mara kati ya China na Iran. Kwa upande mmoja, anataka kutumia na kueneza ujuzi wa matibabu ya jadi ya kichina aliojifunza hapa Beijing katika nchi yake Iran, kwa upande mwingine, amezoea kabisa maisha ya hapa Beijing, na kuwa na upendo wa kina kwa mji huo. Bw. Amirreza amsema,

    "Beijing ni mji wa kupendeza, naupenda sana. Sio mimi peke yangu anayeona hivyo, marafiki zangu wengi wanaipenda sana Beijing, na wamerudi kuishi hapa Beijing, wote wanaipenda Beijing. Sasa mimi, mke wangu na mtoto wangu sote tuko Beijing, na mwanangu anasoma chuo kikuu mjini Beijing. Katika siku za baadaye, natumai kwamba maisha yangu yatakuwa kama hivi sasa, nitaweza kufundisha huku nikitoa matibabu ya akupancha kwa wagonjwa, nusu ya muda wangu niko Beijing, na nusu nyingine nitakuwa nchini Iran."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako