• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali yatoa mwongozo kwa wachina zaidi kuishi miji wanayofanya kazi

    (GMT+08:00) 2016-02-06 18:59:54
    Baraza la mawaziri la China leo limetoa wito kwa serikali za mitaa kusajili wafanyakazi wahamiaji kuwa wakaazi rasmi wa mijini na kutoa wito kwao kununua nyumba mjini.

    Baraza hilo limesema hatua hiyo inakusudia upanuzi wa miji ili kuhimiza matumizi nchini na ukuaji endelevu wa uchumi.

    Baraza hilo linawahamasisha wakulima zaidi kununua nyumba katika miji midogo na ya ukubwa wa wastani iliyo karibu, likiwaahidia mpango mzuri wa kifedha utakaowawezesha watu wenye mapato ya chini kununua makazi pamoja na huduma nzuri zaidi za umma mijini.

    Takwimu zinaonyesha kuwa mwaka 2014 kulikuwa na zaidi ya wafanyikazi wahamiaji milioni 270 ikiwa ni asilimia 20 ya watu wote nchini China. Serikali ya China imepanga kuwasajili wafanyakazi wahamiaji milioni 100 kama wakaazi rasmi wa mijini ifikapo mwaka 2020.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako