• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Australia yapata maendeleo katika kupambana na malaria

    (GMT+08:00) 2016-02-11 21:04:33

    Wanasayansi wa Australia wamepata maendeleo makubwa katika kukabiliana na malaria, ambayo ni moja ya magonjwa yanayosababisha vifo vingi zaidi duniani.

    Utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha Melbourne, kikishirikiana na chuo kikuu cha Stanford na chuo kikuu cha Cambridge umegundua kampaundi mpya inayolenga kimelea cha malaria, ambacho hubebwa na mbu.

    Profesa Leann Tilley aliyeshiriki kwenye utafiti huo amesema, kampaundi hiyo inaweza kushambulia mfumo wa utoaji uchafu wa kimelea cha malaria.

    Matibabu yanayotumika hivi sasa dhidi ya malaria ni dawa mchanganyiko za artemisinin ambazo ufanisi wake unapungua kutokana na virusi kuendelea kuwa sugu kwa dawa hizo. Kila mwaka watu laki 5 wanafariki kwa ugonjwa huo, na asilimia 18 ya vifo hivi ni watoto wenye umri chini ya miaka mitano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako