• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Riek Machar ateuliwa kuwa makamu wa kwanza wa rais

    (GMT+08:00) 2016-02-12 18:48:03
    Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini amemteua Bw Riek Machar kuwa makamu wa kwanza wa rais kufuata makubaliano ya amani yaliyosainiwa mwaka jana. Kwa mujibu wa amri ya rais, makamu wa rais wa sasa Bw James Wani Igga atakuwa makamu wa pili wa rais.

    Makubaliano hayo yalisainiwa Agosti mwaka jana kati ya serikali ya waasi wanaoongozwa na Bw Machar, na yanatambua urais wa Kiir na chama tawala chenye viti vingi vya bunge, asilimia 53 ya mawaziri wa serikali. Kwa upande wa waasi, makubaliano hayo yamewahakikishia nafasi ya makamu wa kwanza wa rais na asilimia 33 ya mawaziri.

    Hata hivyo makubaliano yanakabiliwa na ugumu katika utekelezaji wake hasa baada ya rais Kiir kuamua Oktoba mwaka jana kugawa upya majimbo ya nchi hiyo kutoka 10 hadi 28, uamuzi ambao umepingwa na Bw Machar.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako