• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kundi la uungaji mkono la kimataifa lakubali kusimamisha mapigano Syria

    (GMT+08:00) 2016-02-12 20:07:59

    Wanadiplomasia waandamizi wa kundi la nchi linalojulikana kama kundi la kuiunga mkono Syria ISSG wamekubaliana kuhusu kusimamisha mara moja mapambano kote nchini Syria.

    Baada ya mazungumzo ya siku moja yaliyoandaliwa na Marekani na Russia, wajumbe wa kundi hilo pia wamekubaliana kuongeza utoaji wa msaada wa kibinadamu nchini Syria.

    Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw John Kerry amesema, kusimamishwa kwa mapambano nchini Syria kutatekelezwa ndani ya wiki moja ili kupunguza mabavu na kuruhusu msaada wa kibinadamu kufikishwa kwa raia wa kawaida waliokwama kwenye maeneo ya vita.

    Hata hivyo, Bw Kerry amesema undani wa usimamishaji wa vita ikiwemo njia ya kuusimamia na kuuthibitisha bado haujaamuliwa. Washiriki wa mkutano huo pia wamehimiza kurejesha mazungumzo ya amani ya Geneva.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako