• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapinga ripoti ya Uingereza kuhusu Hong Kong

    (GMT+08:00) 2016-02-13 17:35:11

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw Hong Lei amesema serikali ya China inapinga vikali ripoti inayotolewa na serikali ya Uingereza kila baada ya miezi sita kwa ajili ya kuwasilisha bungeni kuhusu hali ya Hong Kong, na kusema ripoti hiyo ina shutuma zisizo za msingi dhidi ya China.

    Bw Hong Leo amekumbusha kuwa Hong Kong ni sehemu ya China, na mambo ya Hong Kong ni mambo ya ndani ya China, na hakuna nchi yenye haki ya kuingilia mambo ya ndani ya China. Ameitahadharisha Uingereza kuwa makini katika maneno na vitendo vyake na kuacha kuingilia mambo ya Hong Kong.

    Pia amekumbusha kuwa serikali kuu ya China inatekeleza sera ya nchi moja mifumo miwili, na inafuata kwa makini sheria ya msingi ya Hong Kong, na imedhamiria kuendelea kufuata utaratibu huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako