• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ripoti ya UN yasema ukame mkali kusini mwa Afrika umesababishwa na El Nino

    (GMT+08:00) 2016-02-13 17:35:37

    Taarifa ya pamoja iliyotolea na mashirika mawili ya umoja wa mataifa imeonya kuwa, sehemu ya kusini mwa Afrika inakabiliwa na ukame mkubwa uliosababishwa na athari za El Nino.

    Msemaji wa Umoja wa mataifa Bw Stephane Dujarric amesema onyo hilo limetolewa na shirika la chakula duniani FAO na shirika la mpango wa chakula duniani WFP na wadau wengine, kuhusu madhara ya El Nino kwa mavuno katika nchi za kusini mwa Afrika. Mashirika hayo yamesema eneo linalokumbwa na ukame limepanuka na ukame umekuwa mkali zaidi.

    Nchi zilizoathiriwa zaidi ni Zimbabwe, Malawi, Zambia, Afrika Kusini, Msumbiji, Botswana na Madagascar, ambazo msimu huu zimepata mvua chache zaidi katika kipindi cha miaka 35 iliyopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako