• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa usalama wa Munich wafunguliwa huku kukiwa na wasiwasi kuhusu changamoto zinazovuka mpaka

    (GMT+08:00) 2016-02-13 17:35:56

    Maofisa waandamizi wa usalama na ulinzi wamekutana mjini Munich, Ujerumani kwenye mkutano wa mwaka kuhusu usalama, ambao mwaka huu unafuatilia mgogoro wa Syria, wakimbizi, ugaidi na changamoto za kuvuka mipaka. Mwenyekiti wa mkutano huo Bw Wolfgang Ischinger amesema kwa sasa mazingira ya kimkakati ya dunia yako hatarini, na utaratibu wa kimataifa uko katika hali mbaya tangu mwisho wa vita baridi.

    Mkutano huo unahudhuriwa na wajumbe 600 ikiwa ni pamoja na wakuu 30 wa nchi na mawaziri 70. ikiwa ni pamoja na waziri mkuu wa Russia Bw Dimirty Medvedev, Waziri mkuu wa Ufaransa Bw Manuel Valls, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw John Kerry, na katibu mkuu wa NATO Bw Jens Stoltengerg.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako