• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la usalama laihimiza Mali ichunguze shambulizi dhidi ya kambi ya walinzi amani

    (GMT+08:00) 2016-02-13 17:48:19

    Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limetoa taarifa kulaani vikali shambulizi dhidi ya askari wa kulinda amani wa umoja wa mataifa nchini Mali, na kuihimiza serikali ya Mali kufanya uchunguzi kuhusu tukio hilo.

    Taarifa inasema baraza hilo limelaani vikali shambulizi dhidi ya kambi ya tume ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa nchini Mali, ambalo limesababisha vifo vya watu 6 na wengine wengi kujeruhiwa. Baraza hilo limeihimiza serikali ya Mali kufanya uchunguzi mara moja na kuwafikisha wahusika mbele ya sheria.

    Baraza la usalama limesisitiza kuwa, ugaidi wa aina yoyote ni moja ya matishio makubwa dhidi ya amani na usalama duniani. Nchi mbalimbali zinapaswa kufanya juhudi kadri ziwezavyo kukabiliana na matishio ya ugaidi kwa mujibu wa katiba ya Umoja wa Mataifa na sheria za kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako