• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bw. Wang Yi azungumzia matokeo ya mkutano wa 4 wa mawaziri wa mambo ya nje wa kundi la kimataifa linaloiunga mkono Syria ISSG

    (GMT+08:00) 2016-02-13 19:33:11

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amesema, maendeleo makubwa yamepatikana kwenye mkutano wa nne wa mawaziri wa mambo ya nje wa kundi la kimataifa linaloiunga mkono Syria ISSG, na China inapongeza matokeo hayo.

    Bw. Wang Yi amesema matokeo yaliyofikiwa kwenye mkutano huo, kwanza pande husika zimekubaliana kufungua njia ya kusafirisha msaada wa kibinadamu kwa wakimbizi nchini Syria; Pili ni kusimamisha vita nchini Syria ndani ya wiki moja, na kikundi cha kikazi kinachoongozwa na Marekani na Russia kitaundwa chini ya uratibu wa Umoja wa Mataifa, ili kufanya majadiliano kuhusu hatua za kusitisha vita katika siku zijazo; Tatu ni kurejesha mapema iwezekanavyo mazungumzo ya amani ya Syria.

    Bw. Wang Yi ameongeza kuwa, maendeleo hayo hayakupatikana kwa urahisi, na jambo muhimu kwa hatua ijayo ni utekelezaji wa makubaliano hayo. Amesema China ikiwa ni mwanachama wa kundi la ISSG, itaendelea kushiriki kwenye mchakato huo, kufanya kazi za kiujenzi, na kutoa mipango na mapendekezo ili kuhimiza utatuzi wa mgogoro wa Syria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako