• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WHO yasema miezi 18 inahitajika kufanya majaribio ya chanjo ya Zika

    (GMT+08:00) 2016-02-13 19:45:32

    Shirika la afya duniani WHO jana lilitoa taarifa ikisema, uhusiano kati ya virusi vya Zika na ugonjwa wa watoto kuzaliwa kuwa na vichwa vidogo unatarajiwa kuthibitishwa katika wiki kadhaa zijazo, na muda wa zaidi ya miezi 18 bado unahitajika kufanya majaribio ya kimatibabu ya chanjo za Zika, zilizotengenezwa na Marekani na India.

    Msaidizi wa katibu mkuu wa shirika hilo Marie Paule Gini amesema, ukosefu wa ufahamu kuhusu virusi vya Zika umeleta changamoto mbalimbali kwa kazi za utafiti wa chanjo, lakini kutokana na kuwa na uzoefu wa kabiliana na mlipuko wa Ebola, shirika hilo limepiga hatua kubwa katika utafiti wa chanjo ya Zika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako