• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sera ya "kuwa na watoto wawili" yasaidia kuelekea uwiano wa kijinsia

    (GMT+08:00) 2016-03-29 07:47:37

    Tafiti nyingi zilizofanywa zinaonyesha kuwa wanandoa wengi nchini China, hususan kwenye maeneo ya vijijini wanaonyesha wazi kupendelea zaidi watoto wa kiume. Mamlaka ya Takwimu nchini China imesema kuwa, mpaka kufikia mwisho wa mwaka jana, idadi ya watu wanaoishi China bara ilifikia bilioni 1.37, ambao milioni 704.14 ni wanaume na milioni 670.48 ni wanawake. Hii ina maana kuwa, mamilioni ya wanaume huenda wakashindwa kufunga ndoa. Data hizo zinaonyesha kuwa, usawa wa kijinsia ni wanaume 105.0 kwa wanawake 100, na kwa watoto wanaozaliwa ni wanaume 113.51 kwa wanawake 100.

    Kutokana na hali hiyo, China inakabiliwa na changamoto mbili za kuleta uwiano wa kijamii na pia uwiano kwa jinsia za watoto wanaozaliwa. Kimtazamo, ukosefu wa uwiano kati ya watoto wanaozaliwa ni matokeo ya mambo kadhaa, ikiwemo hamu kubwa ya wanandoa kupata mtoto wa kiume, vizuizi vinavyowekwa na sera ya uzazi wa mpango, na shinikizo na gharama ya malezi ya mtoto. Chini ya sera kali ya uzazi wa mpango, wanandoa wengi wanaamua kupata mtoto wa kiume. Profesa wa taasisi ya jamii na idadi ya watu katika Chuo kikuu cha Renming cha China Bw. Zhai Zhenwu anasema:

    "Shinikizo linalowatia wanaume ambao idadi yake ni kubwa kuliko ile ya wanawake litaleta tokeo kwamba wengi zaidi wa wanaume hawajaoa ni wale wanaoko kwenye vijiji vilivyoko mbali, na ndio wale wenye umaskini zaidi. Na una uhakika kuwa katika siku zijazo nchini China watakuwepo wanaume kama hao karibu milinoni 30, hali ambayo tunaweza kutabiri sasa."

    Kuna mambo matatu yanayoeleza kwa nini China inakosa uwiano wa kijinsia, licha ya hali hiyo kuboreshwa katika miaka michache iliyopita.

    Kwanza, ni sababu za kijamii na kiuchumi, hususan utamaduni wa jamii yenye afya, ni msingi wa uwiano wa kijinsia. Elimu bora na kuongezeka kwa uelewa wa hadhi ya kijamii tangu mwaka 2009, vimewafanya wanandoa kuacha kutofautisha kati ya mtoto wa kiume na wa kike. Pia, sera nyingi kama vile kuongeza muda wa kufunga ndoa kwa wanaume na wanawake, mradi wa kitaifa wa wasichana, na kuzuia ngono kwa watoto vimesaidia kwa kiasi fulani, kuboresha usawa wa kijinsia na kupunguza upendeleo wa jinsia, hata unyanyapaa.

    Lakini kutokana na ukweli kuwa uwiano kati ya watoto wanaozaliwa bado hauridhishi, ni dalili kuwa wanandoa wengi bado wanapendelea kupata mtoto wa kiume, na utamaduni mpya wa malezi ya watoto bado haujafahamika. Hata hivyo, uamuzi wa mamlaka wa kuruhusu wanandoa kuwa na watoto wawili, unatarajiwa kurudusha uwiano wa kijinsia kwa watoto wanaozaliwa baada ya kipindi kirefu. Hii ni kwa sababu takwimu rasmi zinaonesha kuwa uamuzi wa serikali uliofikiwa mwaka 2013 wa kuwaruhusu wanandoa ambao mmoja kati yao ni mtoto wa pekee kuwa na mtoto wa pili, ulisaidia kuongeza uwiano wa watoto wanaozaliwa kwa haraka zaidi katika mwaka 2014 na mwaka jana, ikilinganishwa na miaka iliyopita. Kwa kuwa hivi sasa wanandoa wengi zaidi wanatarajia kuwa na watoto wawili, uwiano wa watoto wanaozaliwa unaweza kuboreka zaidi katika mwaka huu. Profesa wa uchumi katika Chuo kikuu cha sayansi cha Hongkong Bw. Lei Dingming ameeleza:

    "Idadi ya wanawake wanaofikia umri wa kufaa kuolewa siyo ya kutosha, huku ile ya wanaume ikiwa kubwa kupita kiasi. Baada ya sera ya "kuwa na mtoto mmoja tu" kuondolewa, hali hii huenda ikatulizwa kiasi."

    Tafiti zinaonyesha kuwa, katika miaka ya karibuni, wanandoa wengi katika maeneo ya vijijini wameonyesha kupendelea kuwa na mtoto wa kiume, kutokana na sera ya uzazi wa mpango, sababu kuu ukiwa ni gharama kubwa ya malezi ya mtoto. Uchunguzi uliofanywa kwenye maeneo ya ndani zaidi ya mkoa wa Guizhou, kusini magharibi mwa China pia unaonyesha kuwa, gharama kubwa ya malezi ya mtoto imekuwa na athari ya kujibana katika familia zenye kipato cha chini kuchagua mtoto wa kuzaa. Watu wanaposhindwa gharama kubwa za malezi ya mtoto kutokana na umasikini, wanapendelea kuwa na mtoto mmoja tu, na wanataka mtoto wa kiume. Hii ina maana kuwa, upendeleo wa jinsia ya mtoto utaendelea kuwepo, alimradi familia masikini katika maeneo yaliyo nyuma kimaendeleo yanashindwa kukabiliana na gharama kubwa za kulea mtoto.

    Mojawapo ya hatua hizo ni sera iliyotolewa hivi karibuni inayowaruhusu wanandoa kuwa na watoto wawili. Sera hiyo sio tu kwamba itasaidia kuleta uwiano wa kijinsia, bali pia itasaidia kuongeza nguvukazi, na pia itaisaidia China kuondokana na changamoto ya ongezeko la wazee katika jamii.

    Kufutwa kwa sera ya mtoto mmoja kunatarajiwa kuongeza watu zaidi ya milioni 30 katika idadi ya watu wanaoweza kufanya kazi itakapofika mwaka 2050, hivyo kusaidia nchi hii kuepuka uhaba wa nguvukazi.

    Takwimu hizo zilitolewa na naibu mkurugenzi wa kamati ya afya na uzazi wa mpango ya China Wang Pei'an. Wang anasema, sera hiyo ya watoto wawili itasaidia kukabiliana na changamoto za idadi ya wazee inayoongezeka kwa kasi. "Idadi ya nguvukazi inatosha kwa sasa, shinikizo la kuwalea watoto nchini China bado halijawa kubwa, na idadi ya watu wanaofikia umri unaofaa kuoa au kuolewa inapungua. Inafaa kutekeleza sera ya "kuwa na watoto wawili" wakati kama huu."

    Bila ya sera hiyo, idadi ya watu wenye umri wa zaidi ya miaka 60 itachukua asilimia 25.7 ya idadi ya jumla ya watu nchini China itakapofika mwaka 2030. Hivyo sera hiyo inatarajiwa kupungua kwa asilimia 2. Wang amesema, ubora wa idadi ya watu, na sio wingi, ndio kitu cha maana zaidi katika hali ya sasa, na kwamba China inahitaji kuboresha ubora wa jamii nzima, hususan nguvukazi.

    Wanasayansi wanasema, idadi ya watu nchini China itaanza kupungua kutoka ile ya kilele ya watu bilioni 1.45 itakapofika mwaka 2030. Wang anasema, bila ya sera ya watoto wawili, anafikiri kuwa mwaka wa kilele unaweza kuwa mwaka 2028.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako