• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe wa bunge la umma la China kwenye eneo la Shijingshan mjini Beijing Yang Guibao

    (GMT+08:00) 2016-03-24 10:20:36

    Mama Wu Baoying mwenye umri wa miaka zaidi ya 70 ameishi katika mtaa wa Yangzhuangbeili ya eneo la Shijingshan mjini Beijing kwa miaka zaidi ya 10. Alipotaja barabara itakayojengwa mbele ya makazi yake, mama Wu anasema,

    "Zamani barabara hiyo ilijaa takataka, sisi wakazi wa maeneo ya karibu na barabara hiyo tunajua ilivyokuwa mbaya. Kwa miaka zaidi ya 10, tatizo hilo bado halijatatuliwa kikamilifu. Lakini sasa tunamshukuru mjumbe Yang Guibao, amesaidia barabara hii kushughulikiwa mwaka huu, tunafurahi sana."

    Barabara aliyotaja mama Wu iko katikati ya mitaa miwili. Wakazi elfu kadhaa wanaoishi karibu, na walimu na wanafunzi zaidi ya 2,000 wanaoishi katika mabweni ya vyuo vikuu vya karibu lazima wapite kwenye barabara hiyo kila siku, na pia kuna shule ya chekechea kando ya barabara hiyo. Ni sehemu yenye watu wengi sana, lakini kwa miaka zaidi ya 10 iliyopita, kulikuwa na barabara moja ya muda yenye upana wa mita 6 tu. Katika miaka ya hivi karibuni, kadiri idadi ya watu na magari yanavyoongezeka, ndivyo hatari za barabarani zinaongezeka. Kwa mujibu wa mpangilo wa mji, kati ya mitaa miwili ilibaki sehemu yenye urefu wa mita 350 na upana wa mita 25 kwa ajili ya kujenga barabara, lakini ilikuwa vigumu kuamua barabara hiyo inapaswa kujengwa na nani na kwa namna gani. Polepole, barabara hiyo ikasahaulika, na ikajaa takataka kila mahali. Mama Wu na wakazi wa huko walitoa malalamiko mara nyingi, lakini walipomwambia mjumbe wa bunge la umma Bw. Yang Guibao, suala hilo gumu hatimaye lilianza kushughulikiwa.

    Bw. Yang Guibao ni mjumbe wa bunge la umma kwenye eneo la Shijingshan mjini Beijing. Baada ya kuambiwa barabara hiyo yenye "utata", aliwasiliana na wakazi wa huko, na baadaye akawasiliana na idara husika kufahamu hali husika ya barabara hiyo, akajulishwa kuwa sababu ya kutofanya ukarabati wa barabara hiyo ni ya utatanishi. Alisema alipoanza kushughulikia suala hilo, hakuwa na uhakika. Bw. Yang anasema,

    "Makazi yalipojengwa hakukuwa na barabara, sasa miaka zaidi ya 10 imepita, kama tunafanya ukarabati barabara sasa, jambo hili litahusiana na maslahi za pande mbalimbali, kwa mfano kuna maoni tofauti kuhusu upana wa barabara na namna ya kuijenga, hivyo ni vigumu kuwahimiza."

    Mitaa miwili kando ya barabara hiyo ilimilikiwa na makampuni mawili ya biashara ya nyumba. Kwa mujibu wa mpango wa wakati ule, makampuni hayo mawili yanapaswa kujenga kwa pamoja barabara hiyo. Lakini baadaye, umiliki wa makazi ulibadilika, na pia hakukuwa na fedha, hivyo ukarabati wa barabara pia ukakwama. Aidha, kwa mujibu wa mpango, hili ni tawi la barabara ya mji lenye kigezo makini cha ujenzi, lakini wakazi wa mitaa hiyo miwili wana maoni tofauti kuhusu upana wa barabara hiyo. Mtaa wa kusini ulipojengwa ulijenga ukuta, ambao upo karibu na majengo, hivyo si rahisi kwa wakazi kupita, hata magari ya zima moto na ya wagonjwa hayawezi kuingia katika hali ya dharura. Kwa hiyo ni lazima kubomoa ukuta huo, lakini ikihamishwa kwa umbali wa mita kadhaa, barabara itakuwa nyembamba. Kwa hiyo ilikuwa vigumu pia kusawazisha maoni tofauti ya wakazi.

    Ingawa hili ni suala lenye utatanishi lililodumu kwa muda mrefu, lakini Bw. Yang Guibao aliamua kutatua suala hilo. Kwanza alisuluhisha maslahi za pande mbalimbali. Mkurugenzi wa kamati ya mtaa wa Yangzhuangbeili bibi Yang Dahong alipokumbuka jambo hilo alisema,

    "Watu wote wanasema kujenga madaraja na barabara ni jambo linalowanufaisha raia, lakini ni vigumu kufanya jambo hilo. Ni barabara yenye urefu wa mita 100 tu, lakini Bw. Yang Guibao alitafuta makampuni husika kuandaa mpango, kusikiliza maoni ya wakazi, alishughulikia jambo hilo kwa mwaka mzima."

    Katika kipindi cha "mikutano miwili" ya eneo la Shijiangshan ya mwaka jana, Bw. Yang Guibao akiwa mjumbe wa bunge la umma kutoka eneo hilo, alitoa mapendekezo kwa serikali ya eneo la Shijingshan kuhusu kufanyia ukarabati barabara. Serikali ilitilia maanani mapendekezo yake, na kuthibitisha kamati ya mpangilio wa mji wa Beijing tawi la Shijingshan kushughulikia mradi huu. Kwa upande mmoja, Bw. Yang Guibao alizialika mara nyingi idara ya mpango, kamati ya uendeshaji wa mji na usimamizi wa mazingira ya mji wa Beijing, na serikali ya mtaa kuwasiliana na wakazi, kujibu maswali yao na ufuatiliaji wao, kwa upande mwingine, Bw. Yang aliandaa idara ya kushughulikia mradi huo kuitisha mkutano maalum ili kuangalia namna ya kukarabati na kujenga barabara hiyo, na kusimamia utekelezaji wa mradi huo. Mkuu wa ofisi ya kutunga mpango wa utawala wa mji katika kamati ya mpangilio wa mji Bw. Tang Fuhai alishiriki kwenye mradi huo. anasema,

    "Mjumbe Yang aliwaalika watu wa kamati ya mpangilio wa mji kuwasiliana na wajumbe wa makampuni husika na wakazi, ili kufahamu zaidi maoni ya watu wote. Alishiriki kwenye kazi ya kutunga mpango, kuhakikisha upatikanaji wa fedha, hatua kwa hatua, na mwishowe kuufanya ujenzi wa barabara hiyo uwe mpango wa utekelezaji wa barabara ya eneo la Shijingshan katika mwaka huu."

    Upandacho ndicho uvunacho. Kutokana na juhudi za Bw. Yang Guibao, hivi sasa ukuta ule umeondolewa, badala yake kuna ukuta mzuri wenye picha za michezo na utamaduni. Takataka hazionekani tena, na barabara iliyofanyiwa ukarabati imekuwa na sura mpya. Fedha zipatazo Yuan milioni 20 kwa ajili ya ujenzi wa barabara zitatolewa na serikali. Barabara hiyo inatarajiwa kuanza kutumika kabla ya mwishoni mwa mwaka huu, ambayo itarahisisha usafiri wa wakazi na kuboresha kwa kiasi kikubwa mazingira ya makazi.

    Bw. Yang Guibao alisema anapoona kuwa amefanikiwa kutatua jambo gumu kwa juhudi zake, huwa moyoni mwake anajivunia kuwa mjumbe wa bunge la umma. Bw. Yang anasema,

    "Unaweza kutatua masuala kwa sababu wewe ni mjumbe wa bunge la umma, na serikali inatilia maanani sana mapendekezo ya wajumbe wa bunge la umma, pamoja na juhudi za pande mbalimbali. Baada ya kutatua suala hilo, najivunia moyoni hata kuliko mafanikio ya kazi yangu yenyewe."

    Bw. Yang Guibao akiwa mjumbe wa bunge la umma kwenye eneo la Shijingshan, siku zote anafuatilia masuala ya maisha ya watu. Mbali na ujenzi wa barabara, Bw. Yang pia anawasaidia wakazi kujenga vifaa vya walemavu, kuondoa majengo haramu karibu na barabara, na kujibu maswali ya wakazi. Kwa maoni ya Bw. Yang, mjumbe wa bunge la umma ni mwakilishi wa raia, ni daraja kati ya raia na serikali, kutoa mapendekezo na sauti za raia kwa serikali; kuwasaidia raia kusimamia serikali, na kuripoti maendeleo ya kazi za serikali kwa raia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako