• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mazoezi ya Yoga yakumbatiwa zaidi na Wachina

    (GMT+08:00) 2016-04-05 07:20:07

    Mazoezi ya yoga hivi sasa yamejipatia umaarufu mkubwa sana hapa China, na pengine kuliko hata mazoezi ya aina nyingine. Yoga ni mchanganyiko wa mazoezi ya kutafakari, vitendo, pamoja na kupumua. Lakini kwa hapa China kuna tabia ya watu wengi sana kufanya mazoezi ya yoga. Na watu hao wanafikia hadi 100.

    Katika siku za Jumapili uwanja wa michezo wa Wusi katika chuo kikuu cha Peking daima umekuwa sehemu inayotumika kufanya mazoezi makali. Lakini hivi karibuni sehemu hiyo imekuwa haina utulivu. Kwani zaidi ya wanaume na wanawake mia tano wanakusanyika katika kiwanja na kufungua mikeka yao na baadaye kusindikizwa na muziki mwororo, wa kutuliza, wakijinyoosha viungo wote kwa pamoja na kubadilisha mikao tofauti. Licha ya joto kali, washiriki wa kila umri wanaonekana wala hawalioni kabisa na kufanya yoga kwa makini zaidi.

    "Kazi yetu kweli ni ngumu sana, lakini tunapofanya mazoezi ya yoga kwa pamoja, akili yangu na mwili unapata kutulia, kitu ambacho kinanifanya nijisikie vizuri sana. Ndio maana naipenda sana yoga mimi pamoja na mwanangu."

    "Nimekuwa nikifanya mazoezi ya yoga kwa miaka mitano sasa. Mimi ni mwigizaji, kazi ambayo ni ngumu sana. Lakini ninapofanya mazoezi ya yoga, mwili, akili, na moyo wangu vinak播放器代码uwa vimetulia sana."

    "Nipo kwenye yoga kwasababu sio tu inanisaidia kuweka sawa hisia zangu, pia ni nzuri kwa mwili. Ni mazoezi yanayohitaji kudumishwa, vinginevyo viungo vyako vinakacha. Madhali unaendelea kufanya mazoezi, basi unakuwa kwenye hali nzuri sana"

    Na hao ni kama tone tu kwenye bahari, wakati ambao maelfu ya mashabiki wa yoga wanaposherehekea siku ya kimataifa ya Yoga katika miji 12 ya China. Kwa mujibu wa Dk Catherine Sozi, Mkurugenzi wa UNAIDS wa China hapa Beijing, yoga tayari imeshakuwa jambo la kidunia.

    "Yoga inatoa njia moja, jumuishi ya kumuendeleza mtu kimwili, kiroho, kiafya na kimaisha. Pia inakuza heshima kutoka mtu mmoja na mwingine na pia katika sayari tunayoishi pamoja. Yoga haibagui. Kwa namna tofauti, watu wote wanaweza kufanya mazoezi, bila kujali nguvu, umri, na uwezo wao."

    Machoni mwa Ashok Kantha, Balozi wa India nchini China, misingi ya yoga inahusu kuunganisha mwili na akili, na mapatano baina ya mtu na maumbile ya asili, mambo ambayo yanalingana sana na utamaduni wa China.

    "Wachina wanajifunza kwasababu wanaona manufaa ya yoga. Jambo la pili ni kwamba pia wanaona namna yoga inavyoendana vizuri sana na utamaduni wao wa China. Tumeona tamasha la yoga tai-chi katika Hekalu la Heaven, na jinsi lilivyoandaliwa vizuri na namna tamaduni mbili zinavyoendana kwenye tukio hilo. Hivyo limepokewa na kukaribishwa, kwasababu yoga inaonekana kama kitu cha kawaida kwa Wachina."

    Anaamini kwamba mazoezi haya yenye asili ya India yanatafuta nyumba yake ya pili katika nchi jirani.

    " Taasisi nyingi za yoga zinaanzishwa hapa China kwa sasa. Hivyo huna haja ya kusafiri kwenda India kujifunza yoga. Juni 13, huko Kunming, chuo cha yoga kilianzishwa, ambacho ni cha kwanza kwa China. Mamia ya studio za yoga, zipo katika maeneo mbalimbali ya China. Yoga imekuwa maarufu kwasababu ya juhudi za watu wa China. Naamini yoga itakuwa harakati za asili nchini China."

    Zhang Hanyu ameendesha kituo cha yoga kwa miaka mingi. Anasema mazoezi yalipoanza kutambulishwa nchini China, yalivutia wanawake wa maofisini tu ambao walitaka kupunguza uzito au kudumisha miili yao. Lakini sasa, watu wanaonekana kutambua manufaa yake.

    "Unapojua mambo mengi zaidi kuhusu yoga, utagundua kwamba yoga sio kuhusu mikao na vitendo. Inakuonesha namna mtu anavyokuwa karibu na ulimwengu wake wa ndani, maumbile, na ulimwengu. Ingawa wachina wengi wanaofanya yoga wanalenga kujifunza mambo yaleyale, lakini kusema kweli yoga ina muonekano wa kushangaza. Inakuonesha manufaa ya pumzi, kutafakari na mtindo mwingine wa maisha. Kutoka vyakula unavyokula, uhusiano wako na watu hadi namna unavyofikiria, yoga inaweza kubadili mambo mengi."

    Leo, mashabiki wa yoga wa China hawaridhishwi na kugeuza viungo na kuzungusha shingo zao tu. Sasa, mawazo tofauti yamechanganywa kwenye mazoezi hayo ya asili ya India.

    Liu Yuezhen ni mwanzilishi wa yoga ya mtindo wa Kichina.

    "Katika suala la vitendo, tumeongezea vitu vya asili vya utamaduni wa China, ikiwemo Tai-chi, Taosim na Confusion."

    Inaonekana Wachina wengi zaidi wataendelea kuchukua mikeka yao na kuikumbatia yoga.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako