• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baba anayesafari na familia yake katika sehemu mbalimbali duniani

    (GMT+08:00) 2016-04-26 06:33:42

    Inaaminika kwamba kusafiri kunaweza kupanua ufahamu wa mtu na kuweza kupata uzoefu mpya wa kina wa utamaduni wa sehemu mbalimbali, lakini imani hii pia inatumika kwa watoto?

    Baba mwenye mtoto wa miaka miwili na nusu anatoa jibu hilo kupitia uzoefu wake binafsi. Bw. Xu Chenghua ni mtu anayetumia muda wake mwingi kusafiri. Xu Chenghua ambaye ni maarufu kwa jina la Lao Ji ni mtaalamu mkubwa wa kusafiri, lakini pia ni baba wa kawaida ambaye ana mapenzi makubwa kwa mwanawe. Akikumbuka alivyojihisi baada ya mtoto wake kuzaliwa anaeleza

    "Nilianza kujua punde tu mtoto wangu alipozaliwa, kwamba nitamrikodi kila kitu afanyacho ikiwemo kulia, kucheka, kudondoka na kukimbia. Pia nilikuwa natamani rikodi yangu ingeanzia siku mbili tu baada ya kuzaliwa kwake, hadi muda atakaokuwa mtu mzima na kuoa. Hapo sasa ndio nitampa tepu hizi za kumbukumbu kama zawadi yake."

    Lao Ji amempa mwanawe jina la Simba, ambaye ni mhusika mkuu katika katuni ya watoto The Lion King. Lao Ji anatamani mtoto wake angekuwa shujaa, mwenye hekima na pia mwenye utaratibu kama alio nao simba kwenye katuni hii.

    Mke wake ambaye amepewa jina la utani la kupendeza "piggy" ni mshirika wake mkubwa katika safari zake. Na wakati mtoto wao alipotimiza miaka miwili mwezi Novemba mwaka 2014, mtaalamu huyo wa kusafiri aliiongoza familia yake ya watu watatu kuanza safari katika Ncha ya Kaskazini. Lao Ji anaelezea mambo aliyokutana nayo katika safari yao hiyo.

    "Katika safari yetu ya kuzunguka dunia, tulikutana na wazazi wengi waliowachukua watoto kwenye safari zao. Pia nimebahatika kuwarikodi wazazi ambao wamemuweka mtoto wao wa miaka mitatu na nusu kwenye kiti cha nyuma cha baiskeli na kumfunga vizuri halafu kusafiri naye, jambo ambalo nafikiri ni gumu zaidi kuliko tunavyofanya sisi. Kusafiri na watoto limekuwa jambo la kawaida siku hizi, ambalo pia linametoa athari kwa wazazi wa China. Miaka mitatu au mine iliyopita, mapumziko ya kifamilia yalikuwa ni jambo la nadra sana nchini China, lakini katika miaka ya hivi karibuni, limekuwa maarufu zaidi."

    Moja ya vitu ambavyo msafiri mtaalamu anavyokusudia kufanya safarini ni kutoa taarifa mara kwa mara kwenye blog zao za safari akiwa safarini. Lao Ji kila mara amekuwa mwepesi wa kutoa habari kwenye chatterbox yake, kwenye blog yake ya Wechat.

    Picha anazoziweka kwenye chatterbox zimemvutia mno rafiki yake mmoja kwenye wechat. Liu Hang ni naibu mkurugenzi wa idara ya programu ya Travel Chanel.

    "Nilivutiwa sana baada ya kuangalia tu picha alizotuma kwenye WeChatter, hususan picha ambayo familia yake inaendesha pikipiki wakiwa safarini. Watu wengi huwa wanaongelea tu kuhusu ndoto hiyo, lakini wachache tu ndio wanaofanikiwa kuitimiza."

    Ikianzia hapa China, familia ya Lao Ji imesafiri duniani kwa kutumia pikipiki yao yenye matairi matatu, kutoka Laos hadi Thailand, Myanmar, Malaysia na Sri Lanka. Ingawa anatumai kuwa atarikodi kila kitu anachohisi kuwa ni cha thamani kwa mtoto wake, Lao Ji amekiri kuwa hana mpango wa kuchukua video za kutengeneza makala.

    "Nilikaribia kupiga video kwa ajili ya documentary kuhusu safari yetu. Wakati wa safari yetu katika nchi tatu hadi nne za kwanza, vifaa vyangu vyote vya kurikodia vilikuwa ni simu ya Iphone 5s na kamera ya GoPro. Hivyo nataka kuwaeleza watazamaji kwamba hiki sio kipindi halisi cha televisheni, ila ni uchunguzi wa baba juu ya ukuaji wa mtoto wake pamoja na kuhisi maumbile ya dunia kupitia macho ya mtoto. Hakuna mwongozaji wa filamu wala mapambano ya bandia kwenye documentary. Filamu hii ina hadithi zetu za kweli."

    Kabla ya familia kuwasili kwenye Arctic, walikuwa wamesafiri jumla ya nchi 13, lakini miongoni mwao Sri Lanka ndio sehemu ya kugeuza.

    Timu ya wataalamu kutoka Travel Chanel ikijumuika kwenye upigaji wao filamu, mfululuzo wa dokumentari za TV kuhusu namna baba alivyokuwa akimpa mtoto wake elimu kubwa kupitia kuona maumbile ya dunia, ikaingia kwenye uzalishaji. Liu Huang anaelezea zaidi.

    "Wakati nawasiliana naye huku nikiwa na shauku kubwa kwenye wechat, alikuwa amesharejea Sri Lanka. Alikubali pendekezo langu la kutuma waandishi wawili nchini Sri Lanka, ambako walikaa pamoja kwa muda wa wiki moja na kufanya mahojiano. Baada ya kuangalia sehemu za video ambazo waandishi wangu walirudi nazo China, na kujua Li Jiao amepiga filamu kitu gani katika safari yake, nikatoa uamuzi hapohapo kwamba tutafuatana nao kwenye safari yao."

    Kuonja vyakula vya kigeni, kusikia lugha tofauti na kutembelea nyumba za nchi nyingine unaweza kuwa uzoefu wa kukufunua macho kwa mtoto na kwa mtu mzima.

    Lakini Lao Ji anafikiri faida ya kumchukua mtoto na kusafiri naye mbali sana na nyumbani ni zaidi ya hii.

    "Kama ningeambiwa niseme kwa ufupi kuhusu nilichofanikiwa kwenye safari hii, ni pamoja na mwanangu kuwa na afya na furaha ingawa ngozi yake imekuwa nyeusi kidogo. Kusafiri kumeipa familia yangu mtazamo mzuri zaidi wa maisha. Sipendi wale watu wanaosafiri muda mrefu ili kukimbia matatizo ambayo wanashindwa kuyakabili. Kusafiri kunaweza kuwafanya watu wawe imara na kufurahia maisha yao zaidi na wakiwa na mtazamo mzuri."

    Dokumentari yenye sehemu mfululizo ya TV, Wild Education au kwa kichina Bie Jiao Wo Bao Bei, imezinduliwa hivi karibuni katika Travel China.

    Lao Ji ameahidi kwamba familia yake itakumbatia safari zaidi na watazamaji wanaweza kutarajia kuona dokumentari zaidi kuhusu safari zao za kushangaza siku za baadaye.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako