• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mchujo wa wagombea nafasi ya katibu mkuu ajaye wa UN waanza

    (GMT+08:00) 2016-04-13 09:26:25

    Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limeanza mchujo wa siku tatu wa wagombea wanane wa nafasi ya katibu mkuu wa Umoja huo akiwemo Igor Luksic kutoka Montenegro akiwa wa kwanza.

    Bw Luksic alijibu maswali ya wawakilishi wa Baraza Kuu kuhusiana na mada za udhalilishaji wa kijinsia uliofanywa na walinzi amani wa Umoja wa Mataifa na utekelezaji wa maendeleo endelevu.

    Alifuatiwa na katibu mkuu wa shirika la utamaduni la Umoja wa Mataifa la UNESCO Bibi Irina Bokova na aliyekuwa kamishna mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi Antonio Guterres.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako