• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yafanya juhudi kuongeza ubora wa uchumi wake ili kujiendeleza na kuendelea kuwa injini ya ukuaji wa uchumi wa dunia

    (GMT+08:00) 2016-04-13 14:45:44


    Mwaka jana, ukubwa wa uchumi wa China ulifikia zaidi ya dola za kimarekani trilioni moja. Kutokana na ongezeko hilo, mageuzi ya muundo wa uchumi wa China yanaathiri sana maendeleo ya uchumi wa dunia na kuyumbayumba kwenye masoko ya hisa ya China pia kuliwatia wasiwasi wachumi wa nchi za nje. Akijibu kuhusu wasiwasi huo kwenye mkutano wa mwaka 2016 wa Baraza la Asia la Boao uliomalizika hivi karibuni, waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang anasema,

    "China iko kwenye mchakato wa kurekebisha muundo wa kiuchumi, ambapo mwelekeo umeanza kutofautiana kati ya sehemu tofauti na sekta tofauti, kwa hiyo ni jambo la kawaida kuwepo kwa matarajio tofauti kwa uchumi wa China katika siku za baadaye, haswa wakati ukuaji wa uchumi wa dunia unapungua hadi kiasi cha chini zaidi katika miaka hii sita."

    Mageuzi ya uchumi ni maboresho ya muundo wa uchumi, ni mabadiliko ya njia za ukuaji wa uchumi, ni kuinuka kwa ngazi ya muundo wa uchumi, ni mabadiliko ya nguzo za uchumi na pia ni mchakato wa kutoka kutafutia ukubwa tu hadi kuzingatia ubora wa uchumi. Mtafiti wa idara ya uchumi wa dunia katika Taasisi ya Uhusiano wa Kimataifa wa Kisasa ya China Chen Fengying anasema,

    "Mbali na marekebisho ya kimuundo, ngazi ya sekta inainuka na mahitaji ya ndani yanaongezeka, tunaweza kuona kuwa mabadiliko ya muundo wa uchumi wa China yanaendelea kwa kasi, na China bado ni nguvu muhimu ya ukuaji wa uchumi wa dunia haswa miongoni mwa masoko mapya yaliyoibuka"

    Mkurugenzi wa idara ya maendeleo ya dunia katika Kituo cha Maendeleo cha Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo OECD Bw. Carl Dahlman anaona kuwa, marekebisho na kuinuka kwa ngazi ya muundo wa uchumi wa China sio tu vinahusisha maendeleo ya China, bali pia vinaathiri kwa kina mwelekeo wa uchumi wa dunia.

    "Tukiangalia ukuaji wa uchumi katika miaka 20 iliyopita, tunaweza kugundua kuwa China ni muhimu kwa ongezeko la uchumi wa dunia, kwa kuwa ukuaji wake wa kasi pia umetoa mchango kwa ukuaji wa nchi zinazonufaika na maendeleo ya uchumi wa China, kama vile zile zinazoendelea. Natolea mfano wa takwimu, katika kipindi cha kuanzia mwaka 1980 hadi 2015, urari wa China kwenye pato la dunia uliongezeka kutoka asilimia 2 hadi 17, hayo ni mafanikio makubwa kwa nchi yoyote inayopata ongezeko la kasi ndani ya muda mfupi. China ni sehemu ya ukuaji wa kasi wa uchumi wa dunia, na kama inaweza kufanikisha mageuzi ya aina mbalimbali, kama alivyosema rais Xi Jinping kwamba uchumi wa China unaweza kuongezeka kwa asilimia 6.5 na zaidi, China itaendelea kutoa mchango kwa ongezeko la uchumi wa dunia. Wakati huohuo, ukuaji wa uchumi wa China utatokana zaidi na ubunifu wa uchumi katika sekta ikiwemo kilimo, huduma na viwanda. Kama China ikifanikiwa, itahimiza maendeleo yake na pia kusaidia dunia nzima."

    Mtafiti wa kituo cha utafiti wa G20 katika Taasisi ya Sera za Kimataifa ya Lowy ya Australia Bw. Tristram Sainsbury pia ana mtazamo ulio sawa na ule wa Bw. Carl Dahlman. Anasema,

    "Ukuaji wa uchumi wa China utapungua, lakini urari wa China katika uchumi wa dunia umeongezeka sana kuliko zamani, kwa hiyo China itaendelea kutoa mchango mkubwa kwa uchumi wa dunia, huu ni mtazamo wangu mkuu. Marekebisho ya uchumi wa China yataendelea, na tunayofuatilia ni udhaifu kwenye ukuaji wa uchumi wa dunia, lakini tuna matumaini mazuri na uchumi wa China."

    Ingawa ukuaji wa uchumi wa China unapungua kutokana na kuhimizwa kwa mageuzi na mabadiliko ya soko, muundo wa uchumi unaboreshwa. Kwa mfano, tangu miaka ya 90 ya karne iliyopita, China ilihimiza ukuaji wa uchumi na uwekezaji katika miundombinu, lakini urari huo unapungua mwaka baada ya mwaka. Aliyekuwa mchumi mwanadamizi wa Benki ya Dunia Lin Yifu anasema,

    "Katika kipindi cha kuanzia mwaka 2006 hadi 2010, ongezeko la uwekezaji lilikuwa ni asilimia 25.5 kwa mwaka, katika kipindi cha kuanzia mwaka 2011 hadi 2015, ongezeko hilo lilikuwa ni asilimia 17.7, lakini mwaka jana ongezeko la uwekezaji lilikuwa ni asilimia 12 tu, hilo ni punguzo kubwa sana."

    Takwimu nyingine pia zinalingana na mtazamo wa Bw. Lin Yifu. Mwaka jana wakati biashara ya uagizaji na uuzaji bidhaa ya China ilipopungua, matumizi yaliongezeka kwa asilimia 10.7 kwa mwaka mzima, na mchango uliotolewa na matumizi kwa ukuaji wa uchumi ulifikia asilimia 66.4, kiasi ambacho ni ongezeko la asilimia 15.4. Waziri wa fedha wa China Gao Hucheng amesema, nchini China, kundi jipya la wanunuzi linaloundwa na tabaka la watu wenye kipato cha wastani na juu limeonekana, ambao wana mahitaji yanayoongezeka kwa bidhaa na huduma bora.

    "Mwaka jana wachina waliokwenda nje ya nchi walikuwa milioni 120, fedha walizotumia kwenye utalii, malazi na manunuzi zilifikia zaidi ya dola za kimarekani bilioni 230, nusu kati yao ilitumiwa na watu wenye kipato cha wastani na juu katika kufanya manunuzi."

    Marekebisho na kuinuka kwa ngazi ya muundo wa uchumi wa China vinaashiria kuwa njia ya ukuaji inabadilika kutoka kutafutia ukubwa hadi kuinuka kwa ubora, na pia vinaonesha kuwa China imeingia kwenye kipindi kipya cha maendeleo yenye kiwango cha juu, na kutoa fursa kwa wafanyabiashara wa ndani na wa nje ya nchi. Mwenyekiti wa kampuni ya Amway ya Marekani Doug DeVos anasema,

    "Katika siku zijazo, uchumi wa China utaendelea kuongezeka kwa nguvu. Kwa kweli siku hizi tunasikia mjadala kuhusu kupungua kwa ukuaji wa uchumi wa China na pia kuna watu wengi wana wasiwasi na jambo hilo, lakini hatuwezi kupuuza kuwa uchumi wa China bado ni imara kwa ujumla, na China bado ni nchi yenye nguvu za kiuchumi, soko la China bado lina uhai, kwa hivyo tunaona imani na maendeleo ya uchumi wa China katika siku za baadaye."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako