• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kijiji chenye wawimbaji wengi

    (GMT+08:00) 2016-04-21 11:31:14

     


    (sauti ya wimbo)

    Wasikilizaji wapendwa, karibuni katika kipindi cha Tazama China. Wimbo uliosikia sasa uliimbwa na wanakijiji wa kijiji cha Tongtou, mkoani Henan. Kijiji hicho kinaitwa "Kijiji kinachoweza kuimba", kwani wanakijiji wake wote wanajua kuimba, karibu kila mtu anaweza kuimba nyimbo zaidi ya 100. Katika kipindi cha leo, tutazungumzia mabadiliko yaliyoletwa na uimbaji kwa maisha ya wanakijiji wa kijiji hicho.

    Mbali na kuimba, wanakijiji hao pia wanaweza kuandika nyimbo na kuigiza opera. Je, kwa nini kijiji hicho kinaweza kuonesha nguvu kubwa ya uhai ya kiutamaduni kama hiyo? Ni kwamba kuanzia mwaka 2008, kijiji hicho kilianza kutekeleza mkakati wa kustawisha kijiji kwa kupitia utamaduni, ili kubadilisha hali ya kuwa nyuma kimaendeleo wakati ule. Hivyo kijiji hicho kiliunda kwaya ya wakulima, ili kuimarisha mshikamano wa wakulima kwa kupitia nyimbo.

    Bw. Dong Junzheng ni katibu wa kamati ya chama cha kikomunisti cha kijiji cha Tongtou ambaye aliingia madarakani mwaka 2008. Anadhani kuwa kijiji kimoja kikitaka kupata maendeleo, kwanza wanakijiji wote wanapaswa kuwa na mshikamano, hivyo hatua ya kuwafanya wakulima waimbe na kucheza ngoma, si kama tu inaweza kuufanya uhusiano kati ya wanakijiji uwe wa karibu zaidi, bali pia inaweza kuimarisha mawasiliano na uaminifu kati ya wanakijiji hao.

    "Zamani kijiji chetu kilikuwa na utamaduni wa kuimba na kucheza ngoma, tangu tulipoanza kufanya mageuzi na kufungua mlango, tuliweka mkazo katika ujenzi wa uchumi, na kuacha utamaduni huo hatua kwa hatua. Hivyo kuanzia mwaka 2008 tuliwakusanya upya wakulima. Niligundua kulikuwa na upungufu wa mawasiliano kati ya wanakijiji, hivyo nilitaka kuboresha hali hiyo kwa kupitia utamaduni. Kuna watu wengi mijini wanaoimba na kucheza ngoma, maoni yangu ni kufanya kama hivyo vijijini, kama kuna nafasi wanakijiji wanaweza kuimba kwa pamoja na kucheza ngoma ili kuzidisha mawasiliano kati yao."

    Mzee Dong Xueshen ana umri wa miaka 70, lakini afya yake bado ni nzuri sana, na anaimba kwaya ya kijiji cha Tongtou. Alisema anapenda sana kuimba, na uimbaji unaleta nguvu kwa watu. Anasema,

    "Zamani kijiji chetu kilikuwa kama michanga, watu hawakujali wengine, hata wakipata matatizo, wakiwa tajiri au maskini, hakukuwa na watu waliowajali wengine. Hivi sasa kwa kupitia uimbaji na ngoma, uhusiano kati ya familia umegeuka kuwa wa karibu zaidi, uhusiano kati ya mama wakwe na wakwe zake umeboreshwa zaidi, na tumekuwa na imani ya kupata maendeleo kwa pamoja. Ujenzi wa vijiji vipya umeboresha sura ya kijiji chetu, shughuli za uimbaji zimeimarisha mshikamano kati yetu, na kijiji chetu kimepata maendeleo ya kasi."

    Mshikamano kati ya wakulima umeimarishwa, wanakijiji wana shughuli za aina mbalimbali za kiutamaduni, Bw. Dong Junzheng amezingatia ujenzi wa uchumi. Kipato kikubwa kwa wanakijiji wa Tongtou kinategemea vijana wanaofanya kazi au biashara mijini, na watu wengine kwa mfano wanawake, watoto, wazee na vijana waliobaki nyumbani wanashughulikia mambo ya kilimo, na chanzo cha kipato chao ni hicho tu. Bw. Dong Junzheng alikuwa anataka kujenga kijiji cha Tongtou kuwa eneo la maumbile la utalii na utamaduni, ili kuwasaidia wanakijiji kuongeza kipato.

    Bw. Dong Junzheng anasema, eneo hilo ni pamoja na bustani maji, bwawa la kuogelea, jukwaa la sanaa la vijiji, eneo la utalii la kuchuma matunda, bwawa la samaki n.k. Hivi sasa zaidi ya asilimia 70 ya wanakijiji wamepata ajira kwenye eneo hilo, hasa eneo la kuchuma stroberi lilileta faida kubwa kwa kijiji cha Tongtou mwaka jana. Anasema,

    "Uwekezaji kwenye eneo la stroberi umefikia yuan laki 2.25 kwa kila hekta, lakini tunaweza kupata yuan elfu 30 hadi 40 kila mwaka. Hivyo tunapanda mazao yanayoleta faida kwetu kama stroberi, ili kuwavutia vijana wengi zaidi kurudi nyumbani na kupata ajira hapa. Tuna imani kuwa utalii wa vijiji unaweza kuwatajirisha wanakijiji wetu, wao hawana haja ya kuondoka nyumbani na kufanya kazi nje. "

    Bi. Li Aiyun amefanya kazi katika eneo la stroberi kwa zaidi ya miaka minne, ana maeneo matatu ya stroberi kwenye eneo hilo. Anafurahi kusema kuwa,

    "Faida ni kubwa, kila eneo linaweza kuniletea faida ya yuan elfu moja hadi mbili."

    Bw. Dong Junzheng anashikilia kujifunza ili aweze kufuata wimbi la maendeleo. Amesema, anataka kutumia mtandao wa Internet ili kukisaidia kijiji cha Tongtou kupata fursa kubwa zaidi ya maendeleo. Anasema,

    "Tumekamilisha tovuti husika, tunataka kuunganisha mtandao wa Internet na kilimo na utalii, kuunganisha wanakijiji na wakazi wa miji, tutaweka ardhi ya wanakijiji kwenye tovuti yetu, tunaweza kuamua aina za chakula au matunda kwa mujibu wa matumaini ya wakazi wa miji na watalii walio na hamu ya kutumia ardhi hiyo. Hivyo wakazi wa miji na watalii wanaweza kula miboga na matunda safi, na wanakijiji pia wanaweza kuongeza kipato. Hii ndiyo njia ya mawasiliano kati ya wakulima na wakazi wa miji, na inaweza kuhimiza uhusiano kati yao."

    Vilevile Bw. Dong Junzheng amesema, anataka kuwavutia vijana wa kijijini kushiriki kwenye ujenzi wa maskani yao, ambao wanaweza kutoa mchango katika kujenga tovuti ya mtandao na wechat.

    Kwa ajili ya ujenzi wa eneo la maumbile, Bw. Dong Junzheng alitoa akiba yake ya pesa. Anasema maofisa wa kijiji hicho wametoa ahadi kwa wanakijiji kuwa, kama eneo la maumbile likipata faida, wanakijiji watapata mgao kutokana na hisa zao, kama eneo hilo halitapata faida, Bw. Dong Junzheng anatumai yeye mwenyewe atabeba hasara, na sio wanakijiji. Anasema,

    "Mimi ni mkulima kutoka kijiji hiki, nataka kuwaongoza wenzangu kutajiri kwa pamoja. Watu wote wakitajiri, kijiji chetu kitatimiza masikilizano."

    Naam, msikilizaji, kufikia hapo ndipo tunapokamilisha kipindi hiki cha Tazama China. Kumbuka tu kipindi hiki kinakujia kutoka Idhaa ya Kiswahili ya Radio China Kimataifa kila Alhamisi wakati kama huu. Katika kipindi cha leo tumezungumzia kijiji cha Tongtou chenye waimbaji wengi, na mabadiliko yaliyoletwa na uimbaji kwa kijiji hicho. Mimi ni Lao Wu, Asante na Kwa heri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako